Propellerads

Thursday, September 22, 2016

mpoma

AJALI YA BASI NA FUSO MOROGORO YAUA 18

Propellerads

AJALI YA BASI NA FUSO MOROGORO YAUA 18 NA KUJERUHI WENGINE 11 LEO





Na Father Kidevu Blog, Morogoro.
WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine  11  wakijeruhiwa vibaya  kwa moto kufuatia magari mawili kugongana ambayo ni Basi Scania mali ya kampuni ya Nganga lililosajiliwa kwa namba T373 DAH  na gari ;la mizigo Mistubishi Fuso T164 BKG.

Ajali hiyo imeelezwa kutokea majira ya asubuhi saa mbili katika Kijiji cha cha Msimba, Tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Polisi mkoani Morogoro kupitia kwa Kamanda wake, Leonald Paulo imesema
 chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo
 kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha 
ajali hiyo. 

Kamanda Paulo aksema basi lilikuwa limepakia pikipiki katika buti na ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basin a lori hilo.

Mbali na abiria waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa na majeruhi takribani 11 walikimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito  Mikumi.

Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliopoteza ndugu na kwa majeruhi na abiria wote. 
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :