PICHA ZA MATUKIO YA AJALI YA MABASI YA J4 EXPRESS NA MWANZA COACH ENEO LA SABASABA WILAYA YA BUTIAMA.
HIVI NDIVYO MABASI YALIVYOGONGANA ENEO LA SABASABA NA KUDAIWA KUSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU WA 29 HADI SASA KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA AWALI.
Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 30 na majeruhi zaidi ya 70 katika eneo la Sabasaba wilayani Butiama.
Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.
Amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani.
Katika hali ya kupishana kutokana na spidi yao hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari hilo dogo lilipaki pembeni baada ya kuona hali tete nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.
