FAHAMU MRADI WA MABASI YAENDAYO KWA KASI UNAOENDELEA KUJENGWA BARABARA YA MOROGORO, DAR ES SALAAM
“Pichani hapo juu unaonyesha mfumo huo utakavyokuwa kwenye eneo la Manzese. Mamlaka inayohusika na usimamizi wa Ujenzi huo ya DARTS wamekua wakitoa maelezo kwa muda mrefu hassa kwenye maonyesho mbalimbali yanapofanuika lakini si aghalabu watu wote kuweza kufika.
Kwa mamtiki hiyo ningependa ndugu wasomaji muelewe yakuwa mfumo huo unaonekana pivhani ndiyo mfumo wenyewe utakavyokuwa, kwamaana kinachoonekana katikati ni kituo ambacho kisingi kitawahifadhi abiria wote wanaokwenda na kurudi mjini (Kariakoo, Posta na Fery) na mabasi yaendayo kasi yatasimama kulia na kushoto mwa kituo kutegemea na liendako.
Usafiri utakuwa ni bora zaidi kwasababu abiria watalipa nauli kabla ya kupanda basi, watapumzika kwenye kituo bila ya kuunguzwa na jua na barabara ya mabasi hayo yatakuwa yakipita yenyewe tu bila kuingiliana na magari mengine na kutoa fursa ya mwendo wa kasi.
Kuhusu magari mengine kama inavyoonekana pichani pembeni kabisa kutakuwa na barabara kwajili ya magari mengine ya kawaida huku kukiwa na sehemu maalum kwaajili ya kuvuka watembea kwa miguu”
****
Blog hii iliweza kutembelea maeneo tofauti ambako shughuli za ujenzi zinaendelea eneo la Ubungo hadi Magomeni chini ya wataalamu wa Kampuni ya STRABAG. Picha zifuatazo zinaonesha baadhi ya matukio ya kazi zinazoendelea..
