Propellerads

Saturday, September 10, 2016

mpoma

habari

Propellerads

 

 

Friday, September 9, 2016

PICHA TANO ZA MUONEKANO WA NDANI WA JENGO JIPYA LA J.K. NYERERE AIRPORT TERMINAL 3 JIJINI DAR

Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, jijini Dar es salaam ambalo bado linaendelea na Ujenzi.
Mafundi wakiendelea na kazi ndani ya jengo (terminal 3).

PROFESA MARK MWANDOSYA AMTEMBELEA NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI.

 Profesa Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya  Idara ya Nishati katika kikao hicho.

TAMKO LA WAZIRI UMMY KWA WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAMKO LA MHESHIMIWA UMMY MWALIMU (MB) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KUHUSU WATOTO WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 09/09/2016
Ndugu Wanahabari, Nitumie fursa hii kupitia kwenu kuongea na watoto wa Tanzania, wazazi / walezi na jamii kwa ujumla katika kipindi hiki muhimu ambacho watoto wetu wamemaliza Elimu ya Msingi. Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza watoto wote waliomaliza mtihani wa Taifa wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu, Hongereni sana!. Ni jambo la ufahari kwetu sisi wote kama wazazi/ walezi na Taifa kwa ujumla kwani hii ni fursa adhimu kwa ustawi na maendeleo ya mtoto na ni moja ya njia ya kutimizwa kwa haki ya msingi ya mtoto ya kuendelezwa ambayo inamjengea mtoto msingi imara wa maisha yake ya baadae. Pongezi zangu nyingi kwa watoto wote wa kike na wa kiume walioweza kufikia hatua hii muhimu kwa maendeleo na ustawi wao.

CHADEMA KUFUNGUA KESI KUOMBA MAHAKAMA KUU KUAMURU JESHI LA POLISI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA KATIKA VITUO MBALIMBALI

 Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta), bila ya kufikishwa mahakamani. Kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni Dar es Salaam leo mchana, wakati akitoa madai ya kushikiliwa kwa wafuasi wa chama hicho zaidi ya 70 wasiofahamika na wengine 10 katika vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya Umoja wa Kupinga Udikiteta (Ukuta). Kulia ni Mwenyekiti Baraza la Umoja wa Vijana Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na kushoto ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.

YALIYOJIRI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Waziri wa Habari, Utaamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akiwaeleza jambo Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Peter Msigwa (Katikati)na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati wa kikao cha bunge leo Mjini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha bunge leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu swali wakati wa kikao cha bunge na kuahidi kuwa serikali kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali nchini ikiwemo upatikanaji wa madawa na vifaa tiba.

MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MH SAMIA WAPATA AJALI

Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

MAKAMU WA RAIS ALIPOTEMBELEA KITUO CHA KUCHAKATA GESI MKOANI MTWARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
 
 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 09.09.2016

KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :