DIRA YA MAFANIKIO
‹ ›
Tabia 8 Muhimu Unazotakiwa
Kuwa Nazo, Ili Kujenga Maisha Ya
Mafanikio Makubwa.
Ni ukweli usiofichika ili uweze kubadili
maisha yako na kuwa ya mafanikio ya
kiwango cha juu ni lazima ubadili tabia
zako ulizonazo sasa na kuwa na tabia
ambazo zitakuongoza kufikia mafanikio
mkubwa zaidi. Unaweza usilione hili
mapema lakini huu ndio ukweli, linapokuja
suala la kutafuta mafanikio vipo vitu vingi
unavyotakiwa kuvifanya na kubadili kama
vile matumizi mabaya ya muda na pesa,
lakini likiwemo na suala la kubadili tabia
ulizonazo ambazo zimekufikisha hapo
ulipo. (Unaweza ukasoma pia Kama
Unataka Kufanikiwa Na Kuwa Tajiri, Acha
Tabia Hizi)
Unapobadili baadhi ya tabia zako
unakuwa unajiweka kwenye mstari wa
kufikia mafanikio yako uliyojiwekea.
Kumbuka, mafanikio yanajegwa na na
tabia ulizonazo, kwa kadri unavyokuwa
na tabia za aina fulani, ndivyo mafanikio
yanakuwa upande wako na kwa jinsi
unavyokuwa na tabia za aina fulani pia
utajikuta ndivyo unavyofukuza mafanikio
katika maisha yako bila ya wewe kujijua.
Ili kujenga maisha ya mafanikio
makubwa unayohitaji, hakikisha
unakuwa na tabia hizi katika masha yako.
1. Tabia ya kuamka asubuhi na mapema.
Unapoamka asubuhi na mapema kabla ya
muda uliojiwekea, kabla ya watu
wengine, unakuwa unapata muda wa
kutuliza akili yako, kujisikiliza wewe
mwenyewe na kupata nafasi ya kutafakari
juu ya maisha yako kwa ujumla. Pia kwa
kuamka asubuhi na mapema sio tu
itakusaidia kukupa muda wa ziada wa
kutafakari juu ya maisha, hiyo itakusaidia
pia kukujengea tabia muhimu ya
kupangilia siku yako mapema, wapi
uanzie na wapi uishie, ambapo tabia hii
itakuongoza kwenye mafanikio. Watu
wengi wenye mafanikio wana tabia hii
muhimu ambayo inawafanya wazidi
kufanikiwa. Ni tabia ambayo unaweza
hata wewe kuwa nayo ili ikuletee
mafanikio mkubwa.
2. Tabia ya kuilisha akili yako kila mara.
Mara nyingi maisha yetu kwa wengi huwa
yametawaliwa na kula vyakula vya kila
aina, hilo unalijua. Lakini kuna kitu
muhimu ambacho huwa haukilishi na
kukisahau mara kwa mara. Kitu hiki sio
kingine ni akili yako. Kama ambavyo mwili
wako unahitaji kula kila siku pia hata akili
yako inahitaji kulishwa tena sana kila
siku. Unahitaji kuilisha akili yako kwa
kujisomea kila siku na hili ndilo hitaji la
msingi unalotakiwa kuwa nalo ili uweze
kufanikiwa. Usiache siku ikapita bila
kwako kujifunza kitu kitakachobadili
maisha yako. Tumia muda wako vizuri
jifunze hata kwa dakika 20 au 30 kwa
siku, baada ya muda utaona mabadiliko
makubwa katika maisha yako. Hii ni tabia
muhimu sana kwako ambayo hutakiwi
kuiacha ili kujenga mafanikio ya kudumu.
3. Tabia ya kufanya mazoezi kila siku.
Hata kama ni kwa dakika kumi na tano
tu, unahitajika kujiwekea utaratibu wa
kufanya mazoezi kila siku. Ili uweze
kufikia mafanikio makubwa unayotaka,
kumbuka unatakiwa kuwa na akili safi
ndani ya mwili wenye afya ya kutosha.
Unapojenga tabia ya kufanya mazoezi
unakuwa unaifanya akili yako iwe nzuri
kiafya na kujikuta ukifikiri vizuri zaidi.
Isitoshe mazoezi yanakusaidia wewe
kupunguza magonjwa hususani ya moyo
na mengineyo mengi ambayo ungeyaweza
kuyapata kizembe, kama ungekaa tu bila
kufanya mazoezi ya aina yoyote ile, hivyo
ni kitu kizuri kwa mafanikio yako
unayoyahitaji.
4. Tabia ya kutekeleza mipango yako
mapema.
Kuweza kuifanya siku yako iwe ya
mafanikio, ni muhimu sana kwako
kujiwekea utaratibu wa kupanga mambo
yako mapema ikiwezekana siku moja
kabla ili kuepuka kuingiliana kwa mambo
ambako kunaweza kukwamisha katika
mipango yako uliyojiwekea. Utaweza
kufanya hivi kwa kuwa na ratiba yako
ndogo ambayo itakuonyesha kwa uzuri ni
nini ufanye katika siku husika inayofuata.
Kuwa na utaratibu huu wa kujipangia
mambo yako mapema utakusaidia wewe
kufanya mambo yako kwa ufanisi na
utalaam zaidi. Ukiwa na tabia hii,
itakusaidia sana kufanikisha mipango
yako mingi uliyojiwekea.
5. Tabia ya kuzingatia mambo.
Haijalishi unakumbana na changamoto za
aina gani sasa, kitu kikubwa
unachotakiwa nacho wewe ni kujifunza
kutenda kwa uzingativu mkubwa
unapotenda mambo yako. Acha tabia ya
kuairisha na kusema ngoja nitafanya
kesho, hii ni tabia ambayo itakukwamisha
na kukurudisha nyuma kila siku. Kama
kuna jambo au kitu ambacho ulitakiwa
kukamilisha leo leo hata kama ni kidogo
ni vizuri ukakamilisha leo ili kesho uingie
kwenye jukumu lingine tofauti. Ili uweze
kujenga mafanikio, ni muhimu kwako
kuwa na tabia ya kuzingatia kila jambo
unalolifanya na unatakiwa ulifanye kwa
ufanisi mkubwa.
6. Tabia ya kuangalia malengo yako upya.
Ni kweli unaweza ukawa una mipango na
malengo mazuri uliyojiwekea, lakini ni
muhimu sana kwako kuwa na tabia ya
kuangalia au kukagua malengo yako mara
kwa mara. Unapokuwa na tabia ya
kukagua malengo yako mara kwa mara,
nakuyapitia tena tena na kuangalia wapi
ulipokosea na wapi ulipofikia inakuwa
inakusaidia wewe kusonga mbele na
kuyafanya malengo yako yazidi kuwa hai.
Hakikisha kila siku unatenga muda kidogo
wa kuyapitia malengo yako upya. Hii ni
tabia muhimu sana mbayo unatakiwa
kujijngea ili kuweza kufikia mafanikio
makubwa yaliyoko mbele yako.
7. Tabia ya kujiamini zaidi.
Hii ni tabia ambayo muhimu pia
unayotakiwa kuwa nayo ili kufikia
mafanikio makubwa katika maisha yako.
Kwa kawaida linapokuja suala zima la
kujiamini kwa wengine huwa ni shida
kidogo. Unaposhindwa kujiamini elewa
kabisa kwako itakuwa ni ngumu kuweza
kufikia kiwango cha mafanikio
unachotaka. Kwa nini inakuwa ngumu
kufikia mafanikio unayotaka? Hii ni kwa
sababu kila kitu ambacho utakuwa
unataka kufanya utakuwa unahisi au
unajiona kama vile huwezi, matokeo yake
utajikuta utakuwa ni mtu wa kushindwa
katika mambo mengi hata kwa yale
ambayo hukustahili.
8.Tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
Kufanya kazi kwa bidii, kuwa king’ang’azi
katika malengo yako ni nguzo muhimu
sana ya kukufikisha kwenye mafanikio
makubwa katika maisha yako. Ikiwa
utaamua kujitoa mhanga na kufanya kazi
zako kwa bidii zote na kujifunza vitu
muhimu kwa kile unachokifanya, elewa
kabisa mafanikio makubwa ni yako. Kama
una nia ya kweli ya kutaka mafanikio
makubwa, chukua jukumu la kujibidiisha
kwa shughuli zako zote unazozifanya.
Matokeo na matunda makubwa utayaona
upande wako kadiri siku zitakavyokuwa
zinaenda mbele. Hata ikifika wakati huoni
matokeo mazuri wewe weka bidii hupotezi
kitu.
Kwa kawaida tabia zetu ndizo zina nguvu
ya kujenga ama kubomoa maisha yetu ya
kila siku. Kama unataka maisha ya
mafanikio, hakikisha unajifunza kujenga
tabia zitakazo kuongoza kwenye
mafanikio ya kweli na sio kukwamisha.
Chukua hatua muhimu za kubadili na
kuboresha maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako
ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA
YA MAFANIKIO kwa kujifunza na
kuhamasika kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA
YAKO YAIMARIKE,
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.
OMG!!!! SECONDARY Teacher Caught Banging Student In Middle Of Classroom On
Snapcha
-
Some serious extra credit going on at this school…
Another teacher busted, this time, there is video proof! A 30-second clip
shows the man humping away on ...
8 years ago