Sehemu ya juu ya jengo la maduka imeporomoka kutokana na tetemeko la ardhi mjini Bukoba Sept 10, 2016
Mtetemeko wa wastani wa ardhi ulokua na nguvu za 5.7 kipimo cha Richter umesababisha vifo vya watu 10 na zaidi ya 100 kujeruhiwa na mamia wengine kukoseshwa makazi.Kufuatana na idara ya Jiolojia ya Marekani, kitovu cha mtetemeko huo ni mji wa Nsunga wilaya ya Kagera, katika eneo la ziwa Victoria, na ulitokea karibu kilomita 10 chini ya ardhi.
Mitetemeko inaripotiwa kutokea umbali wa Kampala, Entebe na Bushenyi nchini Uganda na maeneo kadhaa ya Rwanda na magharibi ya Kenya.
