HUZUNI: KIJANA SAID ALLY ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION HAWEZI KUONA TENA...

"Nianze kuwashukuru ndugu zangu wa Clouds hasa kipindi cha #LeoTena kwa sauti zao mpaka kumfikia ndugu yetu Said ambaye alitobolewa macho kinyama na kwa sasa haoni tena...."Majibu ya daktari yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi. Majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.
"Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam imejitolea k
umpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena."-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira."-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake."-•Vilevile Serikali yetu itatoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kama sehemu ya Mtaji. Kabla ya kupatwa na ulemavu Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwa kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja".
#KutokaOfisiYaMkuuWaMkoa


KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.
