Propellerads

Tuesday, November 8, 2016

mpoma

Kauli ya Mbunge Ridhiwan Kikwete

Propellerads

Kauli ya Mbunge Ridhiwan Kikwete kuhusu wanaosema kabebwa na baba yake

Mwanasiasa Ridhiwan Kikwete amesimama kidete na kusema kuwa hatua aliyofikia kisiasa haitokani na kubebwa na baba yake Dkt Jakaya Kikwete aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ridhiwan Kikwete ni mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambaye kipindi cha uongozi wa Dk. Kikwete alifikia kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Utekelezaji la Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) na kuwa mmoja wa viongozi waliokuwa na ushawishi mkubwa.
Ridhiwan aliliambia gazeti la MwanaHALISI kuwa safari yake ya kisiasa ilianza tangu akiwa na umri wa miaka mitano ambapo alikuwa akipelekwa kwenye shughuli za CCM na Babu yake, Khalfan Mrisho Kikwete.
Alisema kuwa mwaka 1987 baba yake alipoteuliwa kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea walipohamia huko akakuta vijana wa chipukizi na akaamua kujiunga nao.
Siku CCM inatimiza miaka 10 tangu kuanzishwa, babu yake alimpeleka katika sherehe hiyo ambayo alishiriki gwaride la chipukizi na baadae alikutana na Mwalimu Nyerere ambaye alimwambia maneno “Uwe kama baba yako.”
Ridhiwan alieleza kuwa jitihada zake mwenyewe ndio zilizomfikisha hapo lakini watu wasioifahamu historia yake ndio wanaosema kuwa amebebwa na baba yake.
Akizungumzia tuhumwa zinazoelezwa kuwa amejipatia mali nyingi kupitia mgongo wa baba yake, Ridhiwan alikanusha hilo na kusema watu wanaozusha hayo ni wale wenye lengo la kumchafua kwa sababu hakuna mali aliyoipata kupitia mgogo wa baba yake kuwa Ikulu. Marehemu Christopher Mtikila na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Wilbroad Slaa waliwahi kumtuhumu Ridhiwan kujizolea utajiri kupitia mgongo wa baba yake.
Ridhiwan Kikwete alizaliwa 16 Aprili 1979 . Alianza kupata elimu ya msingi katika shule ya Matangini 1987. Elimu yake ya sekondari aliipata katika Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert Dar es Salaam na baadae akajiungana shule ya Mkwawa mkoani Iringa na kumaliza mwaka 20o0.
Akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alifanyakazi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wanafunzi (DARUSO) chini ya Halima Mdee (Mbunge wa sasa wa Kawe, CHADEMA) huku akiwa na nyadhifa nyingine ndani ya UVCCM.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :