MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUADHIMISHWA KESHO.
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTOTAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI TAREHE 1/10/2016
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatoa taarifa kuwa, tarehe 1 Oktoba ya kila mwaka, ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani. Katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku hii kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 49 la mwaka 1991.
Maadhimisho ya siku ya wazee duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) katika kutambua na kuhamasisha jamii kuweza kulinda na kutetea haki za wazee duniani kote. Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa lengo la kutafakari hali ya maisha ya wazee na changamoto zinazowakabili wazee; na hivyo kuweka mipango thabiti ya kuboresha maisha yao na kuwafanya waishi maisha ya heshima, hadhi, na kuthaminiwa utu wao.
Kila mwaka, Maadhimisho haya huwa yanabeba Kauli Mbiu yenye ujumbe mahsusi. Kwa mwaka 2016 Kaulimbiu inasema “Zuia Unyanyasaji dhidi ya Wazee”. Kaulimbiu hii inahimiza Serikali, jamii, na wadau wengine kutafakari na kuweka mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatili, mauaji, ubaguzi na dhuluma dhidi ya wazee; vitendo ambayo ni kinyume dhidi ya haki za binadamu.Maadhimisho haya kwa mwaka 2016 yanafanyika Kitaifa katika wilaya ya Mbalali, mkoani Mbeya. Kilele cha maadhimisho haya kitajumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo huduma ya upimaji wa hiari wa afya na ushauri kwa wazee, michezo na maonesho ya bidhaa na kazi mbalimbali zinazofanywa na wazee.Katika kipindi hiki cha Maadhimisho hatuna budi kuenzi na kudumisha mila na desturi nzuri za kuwaenzi wazee kwa kutambua kuwa wazee ndiyo chanzo cha urithi wa historia ya nchi, washauri wa familia na jamii, watu wenye hekima, na walezi katika jamii. Hivyo jamii inaowajibu wa kuwaondolea vikwazo wazee katika kupata huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua pale ambapo mzee ananyanyashwa au kutendewa isivyostahili.

KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.