| ||
SERIKALI imesema haitasita kuwafukuza wawekezaji,taasisi au mashirika yasiyo ya kiserikali, yanayofanya uchonganishi katika maeneo ya hifadhi na uwindaji.
Aidha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametua Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha nakuagiza kufanyika maridhiano ya kumaliza mzozo kati ya mwekezaji na wananchi wanaozunguka eneo la uhifadhi. Kwa nyakati tofauti, Waziri Nyalandu alitoa msimamo huowa Serikali katika mikutano yake na wananchi katika vijijimbalimbali vya Tarafa ya Loliondo juzi, akiwa katika ziara maalumu ya siku moja mkoani Arusha. Alisema Serikali haitasita kumfukuza mwekezaji yeyote, anayekwenda kinyume cha haki za msingi za wananchi. “Serikali haitasita kumwondoa mwekezaji yeyote ambaye anakwenda kinyume cha haki za msingi zawananchi katika maeneo ya uwindaji. “Mwekezaji ana wajibu wake wa msingi kisheria na wajibu kwa wananchi wa Loliondo,” alisema Nyalandu ambaye hii ilikuwa mara yake ya kwanza kutua Loliondo rasmi kujadili matatizo ya eneo la uhifadhi. “Wananchi nao wana wajibu wao kwa wawekezaji, kwa hiyo pande mbili zina wajibu wa kushirikiana kwawajibu na dhamira zao kwa wanajamii wa Loliondo.” Alisema kwa msingi huo, lazima yawepo mahusiano mazuri kati ya pande husika na kila upande hauna budikunufaika na uwekezaji unaofanyika Loliondo. Hatua ya Nyalandu imetokana na kuwapo kwa uvumi wa kuwaondoa wananchi ili kuwapa ardhi wawekezaji waeneo la hifadhi la Loliondo, Kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC) ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Awali, katika mikutano yake, Waziri Nyalandu alisisitiza kuwa Serikali haina na wala haikusudii kuwafukuza Wamasai wanaoishi katika eneo la uhifadhi la Loliondo. Aliwaambia kuwa taarifa zilizoandikwa na gazeti la The Guardian la Uingereza mwezi uliopita kuwa Serikali yaTanzania inakusudia kuwafukuza wananchi 40,000 ili kumpa ardhi mwekezaji kutoka Falme za Kiarabu, niuzushi na wananchi wa Tarafa ya Loliondo waupuuze. Tarafa ya Loliondo ina wakazi 57,095, kati ya wakazi 174,278 wa Ngorongoro kwa mujibu wa Sensa ya Watuna Makazi ya Mwaka 2012. Aidha, katika mikutano yake, Waziri Nyalandu alielezwa kuwa hakuna boma wala mifugo ya Wamasaiiliyochomwa moto na wanakijiji wanaishi kwa amani. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Raphael Long’oi alisema kimsingi kata tatu katiya saba za tarafa ya Loliondo zimezungumza na OBC kwa nia ya kupata maridhiano, na wamekubaliana. Long’oi alizitaja kata hizo kuwa ni Oloipiri, Maloni na Ololien, na kwamba wananchi wa Loliondo hawawezi kufamasikini, bali wafaidike na rasilimali zao. “Kimsingi hatuwezi kuishi masikini hadi tufe, inabidi tufaidike narasilimali zetu. Tukikaa pamoja na mwekezaji hatuna nia ya kuuza ardhi. “Tukikaa pamoja wengine hawatafaidika kwani wapowanaofaidika na mgogoro. Sisi tunataka maridhiano kwa nia ya kuishi vizuri na kunufaika na rasilimali zetu,”alisema Long’oi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Maloni. Alilalamika kuwa hatua yao ya kuzungumza na kuafikiana na mwekezaji, imezikera kata nyingine, na kuombawasiingiliwe kwani wana uhuru wa kufanya kazi. Kutokana na hilo, Nyalandu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali kuitisha kikao chapamoja cha kata hizo tatu pamoja na kata nyingine nne zilizobaki ili kufikia maridhiano na mwekezaji. Nyalandu aliyefanya mikutano mitatu, aliagiza kikao hicho kifanyike Ijumaa wiki hii mjini Loliondo naatahudhuria. Eneo la uwindaji la OBC limekuwa katika mzozo tangu kumilikishwa kwa ukoo kutoka Falme zaKiarabu, huku wananchi wakivamia eneo hilo. Hata hivyo, inadaiwa kuwa kumekuwapo na uchonganishi na uchochezi kutoka kwa NGO’s na taasisi za kigeni zinazofanya kazi zake Ngorongoro pamoja na wageni hasa wafugaji kutoka nchi ya Kenya. |
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.