Propellerads

Wednesday, October 5, 2016

mpoma

BARNABA ATOA SIRI KUHUSU ANAVYOREKODI MZIKI WAKE

Propellerads

Barnaba Atoa Siri Hii Kuhusu Anavyorekodi Mziki Wake.

  
Msanii Barnaba ametoa siri inayomfanyakusikika na sauti nzuri anapoimba, tofauti na akiongea kawaida ambapo sauti yake inasikika ikiwa kavu yenye mikwaruzo.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya EastAfrica Radio iliyorushwa live kutoka stand ya mabasi ya Makumbusho jijini Dar es salaam, Barnaba amesema yeye kama msanii anatakiwa kuwa tofauti kwenye kazi zake na akiwa kawaida, na pia ni nadra sana kwake kumkuta akiwa anarekodi na haruhusu kabisa mtu amuone akiwa anarekodi.

“Unajua nikija kwenye kuimba nakua mwingine nikiongea mwingine, na hata siku moja siwezi kukuruhusu kunishuhudia nikiwa narekodi, mara nyingi nakuwa narekodi usiku na nakuwa peke yangu, when i’m done nampa file producer, siriya muimbaji anaijua muimbaji, na pia mi naumba sauti yangu, tumefundishwa shule jinsi ya kutoa sauti, jinsi ya kukaa kwenye mic ukiwa unarekodi, so huwezi kunikuta narekodi”, alisema Barnaba.

Barnaba aiendelea kusema kwamba kwa kufanya hivyo anakuwa na uhuru zaidi, na pia watu wengine wanaweza wasimuelewe isipokuwa kwa wasaniii wenzake tu.

“Wanamuziki wananielewa, na siku ukipata fursa ya kuniona narekodi ni nafasi ya pekee, utakuwa umejifunza kitu, ila sio kwa imani mbaya kwani sidhani kama mtu anaweza akachukua sauti yangu, ukumbuke mi nilisoma darasani, kuna vitu ambavyo tunafundishwa darasani,” alisema Barnaba.

Barnaba amekuwa msanii ambaye wengi humsifia kwa sauti yake nzuri anapoimba, lakini watu wengi hushangaa kutokwa na uhalisia wa sauti yake akiwa anaongea kawaida, kwani haifanani na ile inayosikika kwenye muziki wake.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :