Propellerads

Thursday, October 13, 2016

mpoma

HUZUNI: KIJANA SAID ALLY ALIYETOBOLEWA MACHO

Propellerads

HUZUNI: KIJANA SAID ALLY ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION HAWEZI KUONA TENA...

  
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally (anayemfariji juu pichani) aliyetobolewa macho na mtuhumiwa aitwaye Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:
"Nianze kuwashukuru ndugu zangu wa Clouds hasa kipindi cha #LeoTena kwa sauti zao mpaka kumfikia ndugu yetu Said ambaye alitobolewa macho kinyama na kwa sasa haoni tena...."Majibu ya daktari yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi. Majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.
"Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam imejitolea k
umpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena."-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira."-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake."-•Vilevile Serikali yetu itatoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kama sehemu ya Mtaji. Kabla ya kupatwa na ulemavu Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwa kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja".
#KutokaOfisiYaMkuuWaMkoaSaid Ally akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Mhe. Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Mhe. Paul Makonda katika majonzi

KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :