Propellerads

Thursday, October 13, 2016

mpoma

JAMBAZI ALIYEMTOBOA MACHO SAIDI AFANYA VITUKO MAHAKAMANI..LIVE

PropelleradsJAMBAZI ALIYEMTOBOA MACHO MWANANCHI MWENZAKE AWASHANGAZA WANANCHI MAHAKAMANI SOMA ALICHOFANYA LIVE!!

scorpion

Salum Henjewele (34) maarufu kama ‘Scorpion’  mkazi wa Yombo Machimbo anayetuhumiwa kumchoma kisu na kumtoa macho, Saidi Mrisho jana aliwashangaza watu kwa kufanya vituko mahakamani.

‘Scopion’ ambaye ni mwalimu wa mashwati (karate) anadaiwa alifanya tukio hilo Septemba 6 mwaka huu eneo la Buguruni Sheli Jijini Dar es Salaam.
Katika hali ya kushangaza, mtuhumiwa huyo alibadilisha mavazi yake akiwa mahakamani, ili asijulikane mbele ya umati wa watu waliokuwa wamefurika mahakamani hapo. Akiwa anatoka mahakamani ‘Scorpion’ alionekana amevaa nguo tofauti na zile alizokuwa amevaa asubuhi wakati kesi yake ikitajwa.
Awali mtuhumiwa huyo alivaa fulana nyekundu na suruali ya jeans ya bluu, tofauti na mchana ambapo alionekana amevalia baragashia kichwani na shati la mikono mirefu lenye rangi ya kijivu. Mavazi hayo yaliwachanganya baadhi ya watu waliokuwa na shauku ya kutaka kumwona akipanda gari la magereza. Hata hivyo waandishi wa habari na wapiga picha walishtukia ‘janja’ hiyo na kumtambua kwa haraka.
Awali, Scorpion alipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore kwa kuongozwa na  Wakili wa Serikali, Munde Kalombola kwa ajili ya kutajwa kwa shauri la unyang’anyi wa kutumia silaha na kumsababishia upofu wa kudumu, Said Mrisho kwa kumtoboa macho.
Hata hivyo shauri hilo liliahirishwa hadi  Oktoba 19 mwaka huu litakapotajwa tena. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya kesi hiyo namba 276 ya mwaka 2016 ilitajwa kwa mara ya kwanza Septemba 28, mwaka huu. Hata hivyo mshtakiwa huyo jana alionekana mtu asiye na wasi wasi, huku akitabasamu muda wote.
Katika hati hiyo ya mashtaka, ilidaiwa kuwa, Septemba 6 mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, aliiba cheni ya Silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na black bendi ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh 330,000 vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000 mali ya Said Mrisho.
Hati hiyo ilielezwa kuwa kabla na baada ya kutekeleza tukio hilo, mtuhumiwa huyo alimchoma, Mrisho sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo machoni, tumboni na mabegani ili kurahisisha kupata mali hizo.
Mama mzazi wa Mrisho
Nje ya mahakama hiyo, mama mzazi wa Mrisho aitwaye Halima Jissu pamoja na ndugu na jamaa zake walikuwa wakilia muda wote huku wakisema wanamwachia Mungu kwa kilichotokea.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :