KASHESHE YA HABARI ZA PARTY YA SUPER STAR LULU
FAMILIA SASA YA CHARUKA PATI YA LULU
Kulipuka kwa habari kuwa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefanyiwa sherehe na kigogo baada ya kutoka Segerea, Dar kwa dhamana, familia yake imecharuka na kudai kuwa hakukuwa na jambo kama hilo wala haifikirii kufanya hivyo, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Habari za uhakika zilidai kuwa Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mara baada ya kuachiwa kwa dhamana Januari 26, mwaka huu, kuliibuka minong’ono kutoka kwa marafiki zake mbalimbali walioelezwa kuwa walitaka kumfanyia pati lakini ndugu walikataa.
Ilielezwa kuwa licha ya ndugu hao kukataa kumfanyia sherehe ndugu yao (Lulu), bado kuna kikundi cha watu kiliendelea kueneza taarifa za kizushi kwamba lazima kuwe na sherehe ya kumpongeza baada ya kutoka gerezani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya familia ya Lulu zilieleza kuwa taarifa zilizosambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba alifanyiwa bonge la pati na kikundi hicho kama madai ya awali yalivyokuwa, hazikuwa na ukweli wowote na mbaya zaidi zililenga kumjengea Lulu mazingira magumu ya kisheria.
DADA MTU ANENAAkizungumza na paparazi wetu kwa sharti la kutochorwa jina gazetini, dada wa Lulu alisema kuwa familia ilikerwa kupita maelezo na kuwepo kwa taarifa hizo huku akisisitiza kwamba hazina ukweli wowote.
“Sisi kama familia hatujamfanyia wala hatufikirii kumfanyia sherehe ya aina yoyote kwa ajili ya kumpongeza. Tunaomba ieleweke hivyo na hao wanaoeneza habari za uongo waache haraka, hatuzipendi,” alisema dada huyo.
LULU NAE?
Zoezi la paparazi wetu kutaka kumsikia Lulu anazungumziaje juu ya ishu hiyo liligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa kwa sasa amezuiwa kuzungumzia ishu yoyote hasa inayohusu maisha yake katika kipindi hiki anachosubiri kesi yake kuendelea kuunguruma