Propellerads

Monday, October 10, 2016

mpoma

MWANAFUNZI ALIKAMATWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI AACHIWA ARUSHA

PropelleradsMWANAFUNZI ALIEKAMATWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI AACHIWA ARUSHA

      

Image result for mahakama kuu
Na Mahmoud Ahmad Arusha,
Mahakama ya hakimu mkazi Arusha imemwachia huru mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru(CDTI),Allan Mbando baada ya kumwona hana hatia katika kesi ya tuhuma za kufanya uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Mbando,alikamatwa hivi karibuni na jeshi la polisi mkoani Arusha na kisha kufikishwa mbele ya mahakama hiyo kwa kosa la kusambaza ujumbe kupitia Facebook uliosema kuwa”Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote wawe nje ,halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya kukalia kile kiti”.
Akitoa hukumu hiyo jana hakimu mkazi wa mahakama hiyo,Augustine Rwizile alisema kuwa mahakama imemwachia huru mtuhumiwa huyo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake pasipo kuacha shaka yoyote.
Hakimu alisema licha ya kumwachia huru,upande ambao haujaridhika unaweza kukata rufaa.
Mbele ya pande zote hakimu huyo alisema kwamba mahakama imemwachia huru mtuhumiwa huyo kwa kuwa ushahidi uliowasilishwa na upande wa jamhuri hautoshi kumtia hatiani mtuhumiwa huyo na pia hakuna jambo lolote lenye nia ovu katika ujumbe uliosambazwa na mtuhumiwa kwa lengo la kufanya uchochezi.
Hakimu Rwizile alisema kwamba ujumbe uliosambazwa na mtuhumiwa huo haukuwa na umuhimu wowote kwa kuwa
haujaelezea Mwamunyange ni nani lakini pia haujataja nchi husika ambayo ililengwa kupinduliwa.
Hakimu huyo aliiambia mahakama hiyo ya kwamba mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea mkoani hapa ,Moses Mahuna ameachiwa huru na mahakama hiyo kwa kuwa ushahidi uliowasilishwa mbele ya mahakama hauthibitishi ujumbe uliosambazwa mitandaoni ulitoka kwa mtuhumiwa huyo.
“Kwanza ujumbe hauonyeshi ni nani huyo Mwamunyange,pili haujataja nchi inayodaiwa kutaka kupinduliwa lakini tatu ujumbe hauonyeshi jambo lolote la msingi lenye mahusiano ya kisiasa katika taifa linalodaiwa kupotoshwa”alisema hakimu huyo 
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :