Propellerads

Sunday, October 23, 2016

mpoma

TUNZO ZA MTV AFRIKA KUSINI TZ HOI

PropelleradsLeo ndo siku ya utoaji wa tuzo za MTV Mama mwaka 2016 , tuzo hizo zitatolewa nchini Afrika Kusini
Wasanii mbalimbali kutoka Africa wakiwania tuzo hizo.

Tanzania tuna wasanii wetu wakituwakilisha ambao ni...

Raymond - Best breakthrough act

Vanessa Mdeee - Best female artist

Ali Kiba anashare na Sauti sol - Best collabo na song of the year

Navy Kenzo - Best group

Diamond Platnumz - Best male na Artist of year

Ali Kiba na Diamond ni miongoni mwa watumbuizaji kwenye tuzo hizo.

Wale wenye ving'amuzi Dstv kama kawaida, Azam tv nao watakuwa live kupitia azam 1 channel namba 101.

Pia tutaleta updates hapa hapa kila kinachoendelea , zitaanza kutolewa kuanzia majira ya saa 4 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki.

Tuzo za mwaka huu zimetengenezwa na Gold ya kuvutia
1477120505871.jpg


=========

Usiku wa Jumamosi ya October 22 2016 Johannesburg Afrika Kusini ndio siku ambayo zilitolewa rasmi tuzo za MTV Mama 2016 kwa wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2016, mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mkusanyiko wa matukio yote kwenye videos.

Ni kawaida kwa watu maarufu kupewa heshima ya kutoa tuzo kwa kumtangaza mshindi, mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idriss Sultan kutokea Tanzania na msanii na mtangazaji wa TV kutoka Angola Weza Solange walipewa heshima ya kutoa tuzo ya kundi bora.

Msanii wa Bongofleva Alikiba kutoka Tanzania, Sauti Sol kutokea Kenya na mrembo Yemi Alade kutokea Nigeria ambaye pia alishinda tuzo ya msanii bora wa kike walikuwa ni miongoni wasanii waliopewa nafasi ya kuperform.



Wasanii kutoka Tanzania wanaounda kundi la Navy Kenzo Aika & Nahreel walikuwa ni baadhi ya watu maarufu waliopewa heshima ya kutoa tuzo za MTV Mama 2016.



Msanii wa Nigeria Wizkid alipopanda kwenye state kuchukua tuzo yake ya msanii bora wa kiume MTV Mama Awards 2016, tuzo ambayo ilikuwa inawaniwa pia na mtanzania Diamond Platnumz.



Jina la mtanzania Diamond Platnumz lilikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo za MTV Mama 2016, Diamond aliperform wimbo wa Kidogodogo aliowashirikisha P Squre wa Nigeria.

Baada ya baadhi ya wasanii kuperform Partorankig wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Kored Bello, YCEE na Falz wa Nigeria walikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo hizo.

Zamu ya utolewaji wa tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ilikuwa ya msanii wa South Africa DJ Maphorisa akiwa kawashirikisha Wizkid wa Nigeria na DJ Buckz ndio waliofanikiwa kushinda tuzo hiyo ya MTV Mama 2016.

Wizkid hakuishia kushinda tuzo mbili pekee katika usiku huo, lakini waandaaji walikuwa wamemuweka katika list ya wasanii walioperform pamoja na DJ Maphorisa na Emcee.

Msanii Yemi Alade kutoka Nigeria ambaye anafanya vizuri na hit songs zake kadhaa ndio alitangazwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kike ya MTV Mama 2016.

Baada ya kushinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwa mwaka 2016, Wizkid wa Nigeria allitangazwa pia kuwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa mwaka wa tuzo za MTV Mama 2016.

Tanzania safari hii hakuna msanii aliyefanikiwa kushinda tuzo hata moja ya MTV Mama 2016, kwa upande wa tuzo ya Best Breakthrough Act aliyokuwa anawania Rayvanny wa WCB ilichukuliwa na Tekno wa Nigeria wakati tuzo ya chaguo la wasikilizaji iliyokuwa inawaniwa na Yamoto Band ilichukuliwa na Jah Prayzah wa Zimbabwe.

Msanii kutoka United State of America USA Future ndio alikuwa msanii wa mwisho kutoa burudani na kuhitimisha sherehe za utoaji wa tuzo hizo za MTV Mama 2016 kutoka Johannesburg Afrika Kusini. KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :