Yanga kuhamishia mechi zake uwanja wa Amani Zanzibar
Timu ya Yanga imetuma barua ya maombi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar kuomba kuutumia uwanja wa Amani kwenye mechi zake za ligi kuu.
Yanga imechukua hatua hiyo baada ya serikali kuzifungia timu hiyo pamoja na ile ya Simba kuutumia tena uwanja wa taifa wa jijini Dar es Salaam, kwa muda usiojulikana kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mechi yao ya watani wa jadi iliyofanyika Jumamosi iliyopita.
Mechi hiyo ilisababisha hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na mashabiki wa timu hizo kuharibu mali za uwanja huo ikiwemo viti na vitu vingine. Soma hapa chini barua hiyo.