Propellerads

Thursday, November 24, 2016

mpoma

40 wauawa kwenye ajali ya ujenzi China

Propellerads

Watu zaidi ya 40 wameuawa katika ajali ya ujenzi wa kituo kimoja cha umeme huko katika mji wa Fengcheng katika mkoa Jiangxi ulioko kusini mashariki mwa nchi hiyo.
.  Ajali hiyo ilitokea jana usiku wakati jukwa moja lililokuwa likitumika katika ujenzi wa kituo hicho kushindwa kuhimili uzito na kuporomoka. Watu wengine kadhaa pia wamejeruhiwa na wengine kunaswa kwenye vifusi vya maporomoko ya jengo hilo.
Waokoaji wakijaribu kuwaokoa manusura wa ajali ya Zhejiang Oktoba 10,2016
China hushuhudia ajali za mara kwa mara katika vituo vyake vya ujenzi na pia katika migodi ya madini kutokana na kutozingatiwa sheria na hatua za usalama. Oktoba 24 mwaka huu kulitokea mlipuko mkubwa katika nyumba moja huko katika mji wa Xinmin katika mkoa wa Fugu na kupelekea watu 12 kupoteza maisha.  Septemba 27 mlipuo mwingine ulitokea katika mgodi mmoja katika eneo la Ninxia Hui na kuua wachimba migodi 20. Agosti 12 milipuko kadhaa ilitokea kwa kufuatana katika ghala moja la kuhifadhia mada za kemikali huko katika mji wa Tianjin na kupelekea watu 170 kupoteza maisha pamoja na kusababisha hasara kubwa katika eneo hilo. Kufuatia ajali hiyo Rais Xi Jinpin aliwataka viongozi kuchukua hatua za lazima kupunguza ajali za aina hiyo lakini hakuna lolote la maana ambalo limefanyika katika uwanja huo hadi sasa.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :