Kama ilivyo kawaida yangu, jumaclick.com ni kuhakikisha unapata maarifa na kujua vitu vingi kwenye blog hii hii bila kusumbuka. Sasa leo nimeamua kukuletea orodha ya maneno matano (5) ambayo ni makubwa kwa kuwa na herufi nyingi kuliko maneno yote duniani. Kwa bahati mbaya au nzuri vyovyote utakavyopenda maneno yote hayo ni ya kiingereza. Maneno hayo ni kama ifuatavyo;
1. Pneumonoultramicroscopicsilicovolicanoconiosis
Hili ndilo neno linaloongoza kwa kuwa na herufi nyingi, neno huli lina herufi 45 na linamaanisha kuwa ni ugonjwa unasababbishwa na kuvuta hewa yenye vimelea vinavyoshambulia mapafu.
2. Supercalifragilisticexpialiodocious
Hili ni neno la pili kwa kuwa na herufi nyingi, kwa mujibu wa ufuatiliaji wa jumaclick.com neno hilo ndilo neno unalopaswa kutamka ikiwa haujua jambo la kusema. Lina herufi 34.
3. Antidisestablishmentarianism
Kwa mujibu wa jumaclick.com, hili ni neno la 3 kwa kua na herufi nyingi. Likiwa na herufi 29 neno hili linamaanisha kuwa ni upinzani wa wale wanaopinga muingiliano wa mamlaka za kanisa na za nchi.
4. Flaccinaucinihilipilification
Hili ni neno la 4 kwa ukubwa, jumaclick.com tumelifuatilia neno hili na kujua lina maana ya kukikadilia kitu kuwa hakina thamani. Nalo lina herufi 29 kama lilivyo hilo la juu yake.
5. Antitransubstantianalist
Jumaclick.com tumelifuatilia neno hilo na kugundua kuwa lina maana ya mtu anayepinga ukweli kuhusu transubstantion. Neno hili lina herufi 27 na ni neno la 5 kwa kuwa na herufi nyingi.
Hitimisho, huu ni ufuatiliaji wa jumaclick.com, kwa kuwa ufuatiliaji hupingwa na ufuatilijai, tunawakaribisha wafuatiliaji wa mambo kama wataweza watuletee zaidi ya haya. KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.