Mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Nick O’Donoghue ameeleza kuona na kupiga picha taswira ya mtu aliyemuona akitembea juu ya mawingu wakati wa msimu wa Christmas.
O’Donoghue ameeleza kuwa alikuwa anafanya safari ya ndege kuelekea Ireland akipitia uwanja wa ndege wa Gatwick, wakati akiwa angani alishangaa kuuona taswira hiyo ya mtu aliyekuwa anatembea juu ya mawingu.
angani
Baada ya kupost picha hiyo kwenye Reddit, watalaam wa unajim wameanza kutathmini sababu za kutokea kwa taswira hiyo ambayo ilishangaza zaidi baada ya kuonekana kuwa na kivuli kama mtu aliye ardhini.