Propellerads

Sunday, January 1, 2017

mpoma

Watu 35 wauawa mkesha

Propellerads

Watu 35 wauawa mkesha wa Mwaka Mpya Istanbul

Watu wapatao 35 wameuawa kufuatia mashambulizi ya "kigaidi" mjini Istanbul, baada ya mtu aliyevalia kama Santa Klaus kuingia kwenye klabu ya usiku ambako watu walikuwa wakishangiria kuingia kwa Mwaka Mpya.
Türkei Istanbul - Sanitäter transportieren verletzte nach Angriff auf Nachtclub (Reuters/Stringer)
Awali mtu huyo mwenye silaha pia alimuua polisi mmoja na raia aliyekuwa nje ya klabu ya Reina, moja ya maeneo ya kifahari, katika mji mkuu huo wa Uturuki.
"Kwa bahati mbaya, raia wetu 35 wamepoteza maisha yao. Mmoja alikuwa afisa wa polisi. Watu 40 wanapatiwa matibabu mahospitalini," alisema gavana wa Istanbul, Vasip Sahin, akiwa eneo la tukio.
"Mshambuliaji huo - kikatili na bila huruma - aliwalenga watu wasiokuwa na hatia waliokwenda kusherehekea Mwaka Mpya na kufurahi," alisema gavana huyo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Dogan, washambuliaji walikuwa wawili na wote walivalia mavazi ya Santa Klaus, au Father Krismasi. 
Picha za televisheni zilionesha watu waliokusanyika kwenye mkesha huo wa Mwaka Mpya wakitoka kwenye klabu iliyoshambuliwa wakiwa na nguo zao za faragha, huku wakiwa wameghumiwa.
Kwa mujibu wa meya huyo, mashambulizi yalianza saa 7:15 usiku kwa majira ya Istanbul, muda mchache baada ya washangiriaji hao kuuona Mwaka Mpya.
Fadhaa na wasiwasi katikati ya sherehe
Türkei Istanbul - Polizei sichert Nachtclub nach Angriff (Getty Images/AFP/Y. Akgul)
Polisi waliimarisha ulinzi kwenye eneo la mashambulizi na maeneo mengine ya mji mkuu wa Uturuki, Istanbul, muda mchache baada ya mashambuliaji kuwauwa watu wapatao 35 siku ya tarehe 1 Januari 2017.
"Kilichotokea leo ni mashambulizi ya kigaidi," alisema gavana huyo.
Hata hivyo, gavana huyo hakubainisha endapo mshambuliaji naye aliuawa au endapo alikuwa na wenzake wengine.
Watu kadhaa walijirusha kwenye Mto Bosphorus kutokana na fadhaa na juhudi za kuwaokoa ziliendelea kwa masaa kadhaa, kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha NTV. 
Shirika la habari la Digan liliripoti kwamba baadhi ya mashahidi walidai kuwa washambuliaji walikuwa "wakizungumza Kiarabu", huku mtangazaji wa kituo cha NTV akisema kuwa maafisa wa polisi walikuwa wakiendelea na msako kwenye klabu hiyo ya usiku.
Picha za televisheni zilionesha maafisa hao wa polisi wakilitanda eneo hilo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Dogan, kulikuwa na watu 700 waliokuwa wakisherehekea kuanza kwa mwaka 2017 kwenye klabu hiyo wakati inashambuliwa.
Klabu hiyo iko kwenye wilaya ya Ortakoy, moja ya maeneo ya wenye kipato katika mji mkuu huo, na huwa linatembelewa na watu wenye fedha zao tu. 
Uturuki yaendelea kushambuliwa
Türkei Istanbul - Ambulanz und Polizei wegen Angriff auf Nachtclub (picture-alliance/AP Photo/H. Onur Sandal)
Watu wakikimbia kutoka klabu ya usiku ya Reina baada ya mshambuliaji kuwauwa wenzao 35 waliokuwa wakisherehekea Mwaka Mpya.
Uturuki imekuwa ikishambuliwa mara kwa mara, ambapo serikali imekuwa ikiwalaumu wapiganaji wa Kikurdi na wa kundi lijiitalo Dola la Kiislamu. 
Mnamo tarehe 10 Disemba, watu 44 waliuawa kwenye mashambulizi mawili ya mabomu mjini Istanbul baada ya mechi ya mpira wa miguu katika eneo la Besiktas, upande wa pili wa Mto Bosphorus. Mashambulizi hayo, ambayo yalililenga basi la polisi, yalidaiwa kufanywa na wanamgambo wa kundi la Kurdistan Freedom Falcons (TAK) linalotambuliwa kama tawi la msimamo mkali la PKK.
Wiki moja baadaye, wanajeshi 14 wa Uturuki waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mashambulizi ya kujitoa muhanga ambayo nayo yalitajwa kufanywa na TAK yakiwalenga wanajeshi ambao hawakuwa kazini. 
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :