Baadhi ya wanasiasa wakongwe na wafanyabiashara maarufu akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wanashukiwa kujihusisha na madawa ya kulevya.
Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano jijini Dar es salaam, mkuu wa mkoa Paul Makonda ametaja orodha ya watu 65 wanaotakiwa kuripoti polisi Ijumaa wiki hii.
Washukiwa hao ni pamoja na mbunge mstaafu wa kinondoni (CCM), Iddi Azan, mfanyabiashara maarufu, Yusuph Manji, mchungaji Josephat Gwajima na watu wengine binafsi wakiwemo wafanyabiashara wanaomiliki mahoteli, kasino, meli na wamiliki wa vituo kadhaa vya mafuta.