Propellerads

Saturday, September 10, 2016

mpoma

NAIBU WAZIRI ATAJA SABABU ZA WANAFUNZI KUFELI

Propellerads








Naibu Waziri aeleza sababu za wanafunzi kufeli mitihani yao
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema tatizo kubwa linalosababisha wanafunzi kufeli mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne ni kukosekana kwa umakini katika masomo yao.
Akizungumza na walimu na wanafunzi mara baada ya kuitembelea shule ya sekondari Kilolo, Naibu Waziri alisema kuwa changamoto ya ukosefu wa umakini na wanafunzi kutozingatia masomo ndiyo sababu kuu ya kushuka kwa ufaulu katika shule za sekondari nchini.
Alisema mwalimu anaweza akawa amefundisha mada lakini kutokana na wanafunzi hao kukosa umakini katika masomo yao ufaulu wa wanafunzi umekuwa ukishuka. Aliongeza kuwa tatizo kubwa ni kuwa wanafunzi hawasomi na kusababisha ufaulu kushuka.
Naibu Waziri alisema kuwa kutokana na wanafunzi kutozingatia masomo, idadi ya wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na kidatoo cha tano imekuwa ndogo katika shule ya Kilolo.
Mapema, Mkuu wa shule ya Sekondari ya Kilolo bibi Seraphina Chodota alimweza Naibu Waziri kuwa mwaka jana jumla ya wanafunzi 6 walifaulu na kuchaguliwa kuendelea masomo ya kidato cha tano.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :