Wema Sepetu ni mwanamke maarufu si Tanzania tu bali Afrika Mashariki na ana mashabiki wengi zaidi – TeamWema. Tangu awe Miss Tanzania mwaka 2006, mrembo huyu ameendelea kuwa kwenye headlines bila kupunguza.
Umaarufu wake ulichangiwa zaidi na mahusiano yake ya kimapenzi na watu maarufu kuanzia TID, Mr Blue, marehemu Steven Kanumba, Diamond na hivi karibuni, mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan. Lakini niseme kuwa uhusiano wake na Diamond ndiyo uliomulikwa zaidi kuliko mwingine wowote.
Ni katika uhusiano wao, jina la Diamond lilivuma zaidi hasa kwakuwa kipindi wanaanza, Wema alikuwa tayari kwenye kilele cha umaarufu, na hitmaker huyo alikuwa ameanza kuikwea ngazi.
Kwa kipindi chote hicho, Wema amekuwa ni brand kubwa. Wema ni mgodi unaotembea. Hii ni kwasababu hakuna staa mwingine wa kike Afrika Mashariki mwenye kundi kubwa zaidi la mashabiki nyuma yake. Ni kundi kubwa ambalo lipo tayari kumtetea na kumpigania katika nyakati zote, mbaya au nzuri.
Kundi hili limeendelea kuwa aminifu kwake hata pale anapoanzisha uhusiano na mtu mwingine. Lilikuwa nyuma yake kipindi yupo na Diamond na hadi walipoachana. Limeendelea kumfuata kipindi ameanzisha uhusiano na Idris kiasi cha kuifanya couple hiyo itengeneze headlines nyingi ndani ya muda mfupi.
Kwahiyo kwa namna yoyote ile, Wema ni brand inayoweza kuingiza fedha nyingi. Japo alitakiwa kuwa mbali sana kutokana na ushawishi alionao, nafurahi kuona kwamba tayari ameigundua thamani yake na kuanza kuitumia. Napenda kumuona Wema huyu wa sasa ambaye akili yake imefocus zaidi kibiashara na kupush brand yake ya lipstick, Kiss by Wema Sepetu.

KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.