Udhaifu wa Awamu ya Tano usemwe bila kificho
MZUNGUKO mdogo wa fedha uliolikumba taifa hili na maisha ya shida kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali walioanza kuisoma ‘namba’, huku malalamiko yakiongezeka na kutawala kila pande; si ishara nzuri wala mwelekeo wa kueleweka kabisa.
Hali hiyo imeakisi hadi kuifanya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kusikika ikitoa kilio cha kukosekana kwa fedha.
Haya na mengineyo ni miongoni mwa udhaifu unaoonekana wazi kwenye Awamu ya Tano, unao tabiri ishara mbaya isiyo na hila wala kificho kuwa, huko tunakoelekea ni lazima kutakuwa kugumu bila shaka.
Tamko la Rais John Magufuli hivi karibuni la kuwataka wote wanaodhaniwa kuwa wameficha fedha majumbani mwao wazitoe haraka na kuziingiza kwenye mzunguko ni shaka na wasiwasi mkubwa unaoigubika jamii ya Watanzania wasijue la kufanya.
Akitoa agizo hilo rais alisema kwamba la sivyo serikali yake itachapisha fedha zingine mpya ili washindwe kwa kuzipeleka hizo za awali zilizofichwa.
Kauli hiyo aliitoa Septemba mosi mwaka huu jijini Dar es Salaam katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi (ERB) ambao uliwakutanisha wahandisi wa ndani na nje ya nchi ukiwa na lengo la kujadili namna ya kuboresha mazingira ya kazi zao na kutafuta njia sahihi ya kutatua changamoto zao.
Akizungumzia suala na changamoto iliyokuwepo kwa watumishi hewa alisema hivi sasa kuna wafanyakazi hewa na wanafunzi hewa. Kwa Mkoa wa Arusha wamebaini wanafunzi hewa 10,000 na Mwanza 8,000.
“Idadi ya wafanyakazi hewa hadi sasa wamefikia 16,500 kwa miaka yote, nawahakikishia bado kuna wafanyakazi hewa, watafikia 20,500. Hizo ndiyo changamoto kwangu,” alisema.
Pamoja na hali hiyo alisema kuwa mapato ya serikali yameongezeka kutoka asilimia 26 hadi 40.
Bila shaka tamko hilo linaonesha serikali imeanza kutapatapa na sasa inamtafuta mchawi wa mdodoro huo wa kiuchumi ambaye sina uhakika kama serikali itampata mchawi huyo.
Kwa mtindo kama huu, sidhani kama mchawi atapatikana nje ya serikali yenyewe, ambayo ndiyo imekubaliana na hali hii ya uchumi wa nchi ulivyo.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ‘facebook’ aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu ya Serikali (PAC), Zitto Kabwe aliandika maneno haya: “Maajabu ni pale serikali inapotamba kuondoa watumishi hewa zaidi ya 16,000 ili kuokoa matumizi na kusimamisha ajira mpya. Lakini malipo ya mishahara badala ya kupungua yameongezeka kwa bilioni 50 kutoka bilioni 520 kwa mwezi Septemba 2015, jumlisha watumishi hewa na kuibiwa mpaka kuwa bilioni 570 kwa mwezi Juni mwaka huu, bila watumishi hewa na wezi wote wamefukuzwa na waliokuwa wanaishi kama malaika sasa wanaishi kama mashetani. Maajabu ya namna hii yanapatikana Tanzania tu.”
Hapa kuna maswali mengi yaliyotengenezwa na Serikali ya John Magufuli, kiasi cha wananchi wengi kubaki na kigugumizi kwamba ilikuwaje Rais Jakaya Kikwete akaendesha nchi ikiwa na watumishi hewa pasipo malalamiko na kilio cha kupotea fedha?
Idadi kubwa hiyo aliyoibaini Magufuli ya wafanyakazi hewa walikuwepo wakati wa awamu zote zilizopita. Na hasa hii aliyoipokea kijiti ya Kikwete, na safari za nje zilikuwa za mara kwa mara zikiwemo zile za Rais Kikwete mwenyewe; pamoja na watumishi wengine.
Warsha mbalimbali, semina, makongamano na mikutano mbalimbali ilifanyika bila shida. Lakini hakukusikiwa malalamiko kama haya wala matamko kama ya awamu hii.
Lakini tangu aingie madarakani na kuapishwa rasmi Novemba 5 mwaka jana, kuwa rais wa Tanzania. Rais Magufuli, aliingia na kaulimbiu ya ‘Hapa kazi tu!’
Akianza kwa kufuta maadhimisho na sherehe mbalimbali, warsha, makongamano pamoja na semina elekezi. Akisema kuwa hizo zinachangia ufujaji wa fedha bila faida wala maslahi kwa taifa, lakini kama haitoshi akafuta safari zote za nje ya nchi kwa viongozi wa serikali; akisema kuwa watawakilishwa na mabalozi walioko huko.
Hali hii ikaendana na ‘utumbuaji majipu’ ambapo watumishi wa sekta mbalimbali walioonesha kutokwenda na kasi inayoitaka, walitumbuliwa hadharani na kuachishwa kazi.
Halikadhalika suala la ukamataji wa wafanyabiashara waliodhaniwa hawalipi kodi, uliendelea kwa ziara za bandarini za kushtukiza ambapo makontena kadhaa yalikamatwa na kutakiwa kulipishwa ushuru.
Serikali ikajitapa kuwa imefanikiwa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa hakikusanywi hapo awali na fedha zilizokuwa zikiingia mifukoni mwa baadhi ya watumishi wasio waaminifu, kwa maana hiyo tukatangaziwa kuwa pato la taifa limepanda kutokana na kukusanya ushuru mwingi.
Isingetarajiwa kusikia kutoka kwa rais akisema kuwa watu wameficha fedha majumbani mwao na kwenye magodoro yao, hivyo mzunguko wa fedha umekwamishwa na watu hao!
Lazima kuna mahali Serikali ya Awamu ya Tano inakosea. Licha ya kwamba haiwezi kuamua kujishusha na kuuliza uongozi na awamu zilizotangulia ili kuona zilifanikiwaje katika hali kama hii?
Je, serikali inataka wananchi waamini kama kuna baadhi ya watu wanaihujumu ili ishindwe kuendesha mambo yake?
Kuficha fedha ndani kwa lengo gani na kwa maslahi gani na ya nani? Maswali haya ni vema yakapatiwa majibu ya kina ili kutowaweka wananchi njiapanda wakishindwa kuamini hiki kinachoongelewa na serikali.
Kauli hii ya Rais Magufuli haitofautiani na kauli aliyowahi kuitoa mara baada ya sukari kuadimika na wakati fulani kuuzwa kwa bei ya juu, ambapo pia aliwataka wote walioficha sukari kuitoa.