SIKU moja baada ya wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni kurejea katika chombo hicho cha kutunga sheria, wameibua msuguano na wenzao baada ya michango yao katika Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016, kutofautiana na wenzao wengi.
Wanadai kuwa muswada huo hauna maslahi kwa Taifa, bali unalenga kukandamiza uhuru wa kupata habari kama ulivyoainishwa katika Ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema (Arusha Mjini), Pauline Gekul (Babati Mjini), David Silinde (Momba), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Kasuku Bilago (Buyungu) na Mwita Mwikwabe (Ukonga) walioushambulia muswada huo, wakisema una lengo la kuzuia vyombo vya habari visifanye kazi.
Kwa nyakati tofauti, wabunge hao walitofautiana na Muswada huo wakisema hauna maslahi kwa taifa, bali unalenga kukandamiza uhuru wa kupata habari kama unavyoanishiwa katika Ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema “Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.”
Baada ya wabunge wengi waliochangia muswada huo tangu asubuhi kupongeza, Lema alilalamikia muswada huo huku akisema sheria zitawahukumu watu wanaoushabikia muswada huo.
“Kwa wingi wenu mtafanikiwa kuupitisha muswada huu, lakini muswada huu hauna jipya zaidi ya kutaka kuvidhibiti vyombo vya habari ambavyo vinapokea taarifa nyingi sana…vyombo vya habari vikiminywa, sisi wabunge wa upinzani tukiminywa, unadhani kutakuwa na nini hapa? Hakika mshahara wa dhambi daima ni mauti,” alisema.
Gekul naye aliibuka na kuhoji sababu za muswada huo kuitenga Zanzibar, huku akiirudia hoja ya Lema ya kwamba muswada huo hauna nia njema zaidi ya kutaka kufunga watu midomo.
Alikwenda mbali zaidi na kudai muswada huo ukipitishwa na kuwa sheria ipo siku utawaumiza watakaoupitisha. Hali hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kuwashauri wabunge hao kuacha kuwa walalamikaji na badala yake wawe sehemu ya suluhisho kwa kero mbalimbali zinazoelekezwa kwa serikali, wakiwa na wajibu wa kushauri na kutoa mapendekezo yatakayomaliza kero nyingi za Watanzanua.
Aidha, Chenge aliwataka kuacha kuiombea mabaya serikali iliyopo madarakani, ikielezwa mara nyingi ‘Dua la Mwewe halimpati kuku'.
Lakini Chenge baada ya kuombwa Mwongozo na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega (CCM) kutokana na maneno yaliyotumiwa na Lema yakionekana kuupotosha umma juu ya ukweli wa muswada huo, alimtaka mbunge huyo wa Arusha Mjini kuacha kulalamika na badala yake ajenge hoja na pia aje na mapendekezo yanayojenga.
“Lema, acha kulalamika…njoo na mapendekezo. Kufanya shughuli ya kusherehesha Bunge haitasaidia na wala hatuisadii nchi…hivi vijembe havitatusaidia…,” alisema Chenge.
“Dua la mwewe…haya haya,” alisema Chenge na kuamsha vicheko ndani ya Bunge. Ndipo Mbunge wa Madaba, Joseph Mhagama (CCM) alipoibuka na kuwashangaa wanaokosoa muswada huo, akisema wanaikosea haki Tanzania na Watanzania kwa ujumla na kuwakumbusha kuwa, muswada huo haukutunguliwa hewani.
Aliwasihi wausome vizuri na kuwasisitiza kujifunza kwa nchi nyingine duniani na kuuelezea umuhimu wake kwamba ukipitishwa, utaisaidia nchi na wananchi kwani una nia ya kuongeza uwazi, uwajibika na kwamba endapo hivyo vitakuwepo, ni dhahiri nchi itapiga hatua kimaendeleo.
Aidha, alishauri muswada ufanyiwe maboresho ili adhabu kwa watakaopatikana na hatia ya kukiuka sheria waadhibiwe kulingana na uzito wa makosa yao, akisisitiza watakaotoa taarifa zenye madhara kwa serikali na usalama wa nchi, wahukumiwe kifungo cha hadi miaka 20 gerezani kama muswada unavyopendekeza.
Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago, aliegemea katika aina ya adhabu, akisema kwa kuwa muswada huo ukipitishwa, watakaoathirika zaidi ni vyombo vya habari, badala ya kuviadhibu kwa kuvifungia, ni vyema ukaangaliwa uwezekano wa kuadhibu mtu, kwa maana ya mwandishi wa habari au mhariri wake.
Alifafanua kuwa, kufungia chombo kuna madhara makubwa kutokana na vyombo husika kuajiri watu wengi, hivyo ni bora adhabu iangukie kwa aliyesababisha kosa na si taasisi.
Aidha, alishauri muda wa kuomba taarifa upunguzwe kutoka siku 30 hadi kulingana na mahitaji ya mhitaji wa taarifa, akijenga hoja kuwa, taarifa nyingi zinaweza zisiwe na maana endapo zitapatikana nje ya muda.
Katika mjadala ulioendelea tena jana, wabunge waliendelea kuupongeza muswada huo, huku baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani wakionekana kuupinga kwa kile walichodai itageuka sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari.
Mbali ya Kamati za Bunge na Serikali, wadau wengine waliotajwa kuwasilisha maoni yao katika muswada huo na kuridhishwa kwa kiasi kikubwa na mapendekezo yake ni pamoja na Mahakama, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Muungano wa Katiba Tanzania (JUKATA) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Wadau wengine ni Sekretarieti ya Msaada wa Sheria, Wizara ya Kati, Sheria na Taasisi ya Habari ya Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT).
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.