AJALI MBAYA ILIYOWAHI KUTOKEA MIKESE MOROGORO LEO ASUBUHI
Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund
Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea
Mlipuko mkubwa wakati matenki ya mafuta yakilipuka
Askari wa kikosi cha zimamoto wakijaribu kuuzima moto huo