Lady Jaydee: Sijawahi kuwa na uhusiano na msanii
Lady Jaydee ameweka bayana kwamba hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.
Alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV wakati akizindua video ya wimbo wa ‘Ndindindi.’
Katika mahojiano hayo pia Jide alisema yeye ndiye msanii wa kwanza kuwahi kufanya interview na Justin Campos
“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya ‘Njalo’ nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama ‘Mina Nawe’, Justin ndio alikuwa dwa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanya naye kazi tena 2016,” alisema Jaydee.
Ndindindi utapatikana kwenye album yake mpya iitwayo Woman.