Juma Nature amefanya mambo makubwa kwenye muziki mpaka akina Diamond wakajulikana – Jay Moe
Wakati wasanii mbalimbali Ijumaa hii wakiposti picha za Juma Nature na kum-wish katika siku yake ya kuzaliwa, rapper Jay Moe amewataka wadau mbalimbali wa muziki kuheshimu harakati za mgongwe huyo ambazo zimesaidia kuutangaza muziki wa bongofleva kitaifa na kimataifa.
Jay Mo amesema wataendelea kumheshimu Juma Nature kwani vitu ambavyo amevifanya, ndivyo vimesababisha wasanii kama kina Diamond kujulikana kimataifa.
“Tutamkumbuka kwa kufanya vitu ambavyo vimewafanya mpaka kina Diamond wakajulikana,” Jay Moe alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio. “Muziki anaoimba Juma Nature ni ule muziki wa watu wa chini, amegusa maisha ya watanzania halisi, unajua sisi hata kama tulikuwa tunafanya muziki lakini haikuwa kama ya Juma Nature,”
Aliongeza, “Kipindi hicho unaenda kwenye show ya Juma Nature unakuta watu wanapanga foleni ndefu kukata tiketi, alikuwa anaweka kiingilio cha chini ili kila mtu aweze kuingia, hajajichukulia mi super star na kuvaa ukinondoni au Ilala, muziki wake ulikuwa umelalia maisha ya mtaa na watu wengi, alikuwa mjanja kutarget hawa watu wenye uwezo wa chini kimaisha”,
Jay Moe amesema kutokana na aina hiyo ya muziki wa Juma Nature, ndiyo ume’inspire’ vijana wengi na kufuata nyayo zake.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.