Propellerads

Friday, October 14, 2016

mpoma

MAKONDA AMETOA MILIONI KUMI WA KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO

Propellerads

MAKONDA ATOA MILIONI 10 KWA ALIYETOBOLEWA MACHO.

  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Said Ally, ambaye ametobolewa macho na Mkewe Zara Sudi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari.

Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii.SIKU chache mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kosa la kumtoboa macho ndugu, Said Ally wa Buguruni kwa Mnyamani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ameamua kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake za zote za matibabu na mtaji wa Shilingi Milioni kumi.
Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kijana huyo kufika katika ofis za mkoa , Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeonekana kuwa bado Said atoweza kupata tena nafasi ya kuona tena hivyo anahitaji matibabu ya ziada.“Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.
Kwa upande Ndugu Said Ally amesema kuwa anawashukuru madaktari kwa juhudi zote walizofanya na shukrani kubwa sana ziende kwa Gea Habibu wa Clouds Media na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa moyo wake aliounyesha kwa kujitoa kwa hali na mali.
“Kiukweli nimeona Mungu akiwa katika upande wangu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na watu wa Clouds na madakatari naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu” alisema Said.Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kumsaidia BwanaSaid Ally ambaye alitobolewa machi jijini Dar es Salaam
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :