Propellerads

Friday, October 14, 2016

mpoma

MUENZINI NYERERE KWA KUFANYA KAZI

PropelleradsMuenzini Nyerere kwa kufanya kazi


 
WATANZANIA wamepewa wito kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa kufanya kazi, ili kuiletea nchi maendeleo.
Mwito huo ulitolewa jana na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi mstaafu, Job Lusinde, alipozungumza kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa na kuambatana na shughuli za usafi.
Aliwataka vijana kuacha kubweteka na badala yake kufanya kazi kwa bidii, ili kulikwamua taifa kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuwatumikia wananchi.
“Wakati wa Mwalimu watu walikuwa wakichapa kazi, hata kwenye ofisi habari za njoo kesho ilikuwa hakuna, hata wakati tunapata Uhuru, ilikuwa Uhuru na Kazi, Imani na Umoja vilikuwa vikiongozwa kwenye nembo. Leo tunashukuru baada ya Uhuru na Kazi sasa ni Hapa Kazi Tu,” alisema Balozi Lusinde.
Alisema Mwalimu alikuwa akipenda kila mtu afanye kazi, alikuwa ni mtu mwenye upeo mkubwa, hakupenda makuu na kwamba aliishi kama mtu wa kawaida na hakupenda ufahari.
“Kama ulitaka kumuudhi Mwalimu muoneshe ufahari, alikuwa mtu asiyependa makuu, tulijikuta tunafanya naye kazi vizuri kwa sababu tulimuelewa,” alisema.
Alisema alikuwa akipenda kuwapa uongozi wachapa kazi na anao waamini ili wamsaidie katika kazi za kulijenga taifa.
“Mimi nilipata uwaziri katika Baraza la Kwanza la Mawaziri nikiwa na miaka 30, tulikuwa 12 akiwemo Mwalimu Nyerere,” alisema.
Alisema kati ya Mawaziri hao 12, 10 wamefariki dunia na kubaki yeye na Sir George Kahama. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christine Mndeme alisema, “huu si wakati wa kulala bali kila mmoja achape kazi kwani hata Baba wa Taifa alituhakikishia uhuru na kazi”.
Alisema Serikali wilayani Dodoma na Jeshi la Polisi wilayani humo viko imara kuhakikisha vinakabiliana na vitendo vyote vya uhalifu. Pia aliwataka wananchi kutunza mazingira. Alisema atakayekamatwa akitupa takataka hovyo au kujisaidia hovyo atatozwa faini Sh 50,000 kwa kila kosa
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :