Propellerads

Thursday, October 6, 2016

mpoma

MKOA WA MARA NA MATUKIO KATIKA PICHA

PropelleradsMKOA WA MARA NA MATUKIO KATIKA PICHA

Hili ni daraja la Kyarano, barabara itokayo Nyamuswa, Wilayani Bunda, kupitia Butiama, kwenda Musoma, mkoa wa Mara,, Magari hupita eneo hili kwa shida hususan wa mvua kama inavyooneka  
Hapa jitihada za Serikali kujenga barabara kwa kiwango cha lami daraja la kisasi zikiendelea kama inavyoonekana katika picha hii.
Hii ni barabara ya vumbi, inayopita katikati ya mji wa Butiama, nyumbani kwa muasisi wa Taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mtoto huyu mdogo, ambaye alipaswa kuwa darasa la shuleni, akifanya kazi ngumu ya kusomba matofali tena kwa umbali mrefu kama alivyonaswa na kamera yetu eneo la Butiama, mkoani Mara.
Inasikitisha kwa mzazi wa mtoto huyu kumwachia au kumtuma kufanya kazi ngumu kama hii, atawezaje kufanya vizuri katika masomo yake iwapo ataanza shule au kama ameanza shule.

Huu ni Mlima maalumu unaodawa kuoteshwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ulioko Butiama mkoani Mara.
Bibi huyu alikutwa na kamera yetu akiwa kando ya barabara iendayo Musoma, katika Stendi ya Butiama, akiwa na mjukuu wake wakisubiri usafiri.
Watoto hawa wadogo ambao walipaswa kuwa shuleni walikutwa na kamera yetu wakisomba maji katika kijiji cha Busegwe, kilichoko, Wilayani Butiama, Mara

Hapa wakishangaa kamera baada ya kugundua wanapigwa picha.
Hapa wakijaribu kuondoka
Mama huyu alikutwa na kamera yetu akiwa na watoto wake ambao walipaswa kuwa shule wakati huo. Hapa wakitoka shambani.
Serikali ya Awamu ya Nne imedhamilia kuwashitaki wazazi watakashindwa kupeleka watoto shule, kwani elimu sasa ni bure, hakuna visingizio.

Watoto hawa wadogo walikutwa wakitoka kutafuta kuni, katika eneo la Butuguri, Wilaya ya Butiama.
Huyu mwanafunzi kutokana na sketi aliyovaa kuwa ya shule, lakini alikuwa akitoka porini kutafuta kuni, badala ya kwenda shule.
Hali ya barabara kutoka mjini Musoma kwenda Nyamuswa kupitia Butiama ikiwa katika hali mbaya, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Magari yakipita kwa shida katika barabara hii
Baada ya kutafuta kuni, watoto hawa wakivuka sehemu ya daraja lililoko Butuguri ili kuelekea nyumbani.
Huyu akifua nguo kando ya daraja lililoko Butuguri
Watoto hawa wameacha shule na kusafiri mwendo mrefu kwa ajili ya kutafuta mashine ya kusaga nafaka
Hapa wakivuka sehemu ya daraja linalojaa maji

Hapa ni Kijiji cha Makutano, maarufu kwa jina la Ziroziro, njia panda ya Tarime, Sirari kwenda nchi jirani ya Kenya, watoto ambao walipaswa kuwa shule wakifanya biashara kwenye magari ya abiria.
Mjini Tarime ambapo Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani alimkamata mwendesha Bodaboda. Hata hivyo alilazimika kumwachia baada ya wananchi kumzonga.
Hapa Askari huyo akiongea na mmoja wa wananchi hao.
Akina Mama wakifanya biashara ndogondogo katika kituo cha mabasi Tarime.
Mabasi yakisubiri abiria katika mji wa Tarime
Mtoto huyi akifanya biashara ya kuuza vitunguu katika stendi ya Tarime.
Daraja la kisasi la Kirumi, lililoko Mto Mara.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :