NIGERIAYABADILI MBINU ZA KUKABILIANA NA BOKO HARAM
Duru za usalama nchini Nigeria zimearifu kuwa, serikali ya nchi hiyo imebadili siasa zake za kiusalama kwa ajili ya kukabiliana na vitisho vya kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria kumteua Mohammed Usman kuwa mkuu wa idara ya usalama na ulinzi ya nchi hiyo. Weledi wa mambo wanaamini kuwa hatua ya Rais Buhari ina lengo la kubadili siasa kuu za kupambana na Boko Haram ambapo sasa zitajikita katika kukusanya ripoti za kiintelijensia kama njia pekee ya kukabiliana na wimbi la vitisho vya kiusalama kutoka kwa wanachama wa kundi hilo. Kabla ya hapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Geoffrey Jideofor Kwusike Onyeama, sanjari na kuashiria ongezeko la mashambulizi ya wanachama wa Boko Haram alisisitiza kuwa, kile ambacho hii leo kinatakiwa kufanywa na jeshi la nchi hiyo ili kulishinda kikamilifu genge hilo ni kutekelezwa kwa operesheni za kiintelijensia nchini. Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, vitendo vya ukatili na mauaji nchini Nigeria vimeiweka nchi hiyo katika nafasi ya nne miongoni mwa nchi za dunia zenye idadi kubwa ya watu waliouawa na kujeruhiwa katika wimbi la machafuko ya mwaka 2015, baada ya Syria, Yemen na Iraq.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.