WAZIRI MKUU ATAKA ORODHA YA WADAIWA SUGU DUWASA: Ni wa taasisi za umma, wanadaiwa sh. bilioni 1.4
WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza apatiwe orodha ya wadaiwa sugu wa taasisi zote za Serikali mkoani Dodoma ambao wamelimbikiza deni la sh. bilioni 1.4 zikiwa ni bili zao za maji.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 2, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) mara baada ya kukagua utendaji kazi wa chanzo cha maji cha Mzakwe nje kidogo ya mji wa Dodoma. “Niletee haraka orodha ya wadaiwa wote wa Ofisi za Serikali na taasisi za umma ambao hawajalipa bili zao. Madeni yote ni lazima yalipwe,” amesema Waziri Mkuu. Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya siku mbili ya kukagua maandalizi ya Serikali kuhamia Dodoma, anatembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za jamii pamoja na kukagua miundombinu ya mkoa huo.

KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI.