Propellerads

Friday, October 21, 2016

mpoma

ZITTO KABWE NA MH: NAPE WALIVYOJIBIZANA

PropelleradsTIZAMA ZITTO KABWE NA MH NAPE WANAVYOJIBIZANA KUHUSU MUSWADA MPYA WA HABARI TANZANIA

http://www.thecitizen.co.tz/image/view/-/2860938/medRes/1112412/-/f2ladnz/-/Zitto+Kabwe+Photo.jpg
Baada ya Jana Mbunge wa kigoma Mjini Kuandika Waraka akikosoa Muswada wa Huduma za habari 2016 Unaowasilishwa Bungeni Hatimaye Waziri mwenye Dhamana ya Habari na michezo Mh Nape Nnauye aliamua kumjibu Mh Zitto lakini Baada ya majibu hayo Tayari mh  Zitto Kabwe ameandika waraka mwingine akikosoa majibu ya waziri huyo.Tizama Mtiririko wa Majibizano hayo

Zitto Kabwe Serikali ya awamu ya Tano imewasilisha Bungeni Muswada wa Sheria kutunga Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari. Muswada wa Sheria hiyo sasa upo mbele ya kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa na kisha kuwasilishwa Bungeni. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kanuni ya 84 Kamati ya Bunge inawajibika kuutangaza muswada na kupokea maoni ya wadau mbali mbali. Kwa hakika wadau wa muswada huu ni wananchi wote kwani haki ya kupata habari ni haki ya kikatiba.

 Hata hivyo, waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari na mitambo ya kuchapisha magazeti na majarida ni makundi yatakayoathirika moja kwa moja na muswada huu utakapokuwa sheria. Hata hivyo, muswada unapelekwa mbio na mwenyekiti wa Kamati katishia kuwa iwapo wadau hawatatoa maoni, Kamati yake itaendelea na kazi zake za kutunga sheria.

Kwa muda mrefu sana Waandishi wa habari na wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakitaka kuwepo na sheria ya kusimamia tasnia ya habari. Ninaambiwa kuwa juhudi za kutunga sheria hii ni mchakato wa zaidi ya miaka 20, tangu mwaka 1993 ambapo muswada wa kusajili waandishi wa habari uliondolewa Bungeni baada ya kuwasilishwa na Dr. William Shija wakati ule akiwa Waziri wa Wizara ya Habari na Utangazaji, ambaye sasa ni marehemu. 

Vile vile kumekuwa na kilio kikubwa cha vyombo vya habari kufungiwa kwa kutumia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo inampa mamlaka makubwa sana waziri wa Habari. Wananchi wengi na wapenda demokrasia walitaraji kwamba sheria mpya ingeweza kuondoa sheria kandamizi na kuweka uhuru wa vyombo vya habari ipasavyo. Hicho sicho kilicholetwa na Serikali ya Rais John Pombe Magufuli.

Muswada uliopo mbele ya kamati ya Bunge unatoa tafsiri pana sana ya vyombo vya habari. Sehemu ya 3 ya Muswada inatamka chombo cha habari ni pamoja na gazeti, kituo cha radio na televisheni ikiwemo mitandao ya kijamii ( online platforms). Muswada unatamka kuwa ni lazima ‘media house’ iwe na leseni maalumu kwa ajili kufanya kazi na waandishi wa chombo hicho ni lazima waandikishwe kwenye chombo kiitwacho Accreditation Board ( Bodi ya Ithibati). Iwapo sheria hii itatungwa maana yake ni kwamba mtandao kama wa jamiiforums utapaswa kuandikishwa na watu wote wanaotoa maoni yao kwenye mtandao huo lazima wawe na ithibati! Haitaishia hapo, bali hata blogs nk zitapaswa kuandikishwa kama ilivyo magazeti. Hatua hii itaminya sana uhuru wa watu kupata habari na kupashana habari. Hata uhuru wa kujieleza utaminywa sana kupitia mitandao ya kijamii.

Muswada unataka kuwepo na sheria ya Serikali kuamua vyombo vya habari viandike nini na vitanagze nini. Sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa Taifa. Itakumbukwa kwamba muswada uliopita ambao ulikataliwa ulitaka ifikapo saa mbili usiku televisheni na radio zote ziungane na TBC kutangaza taarifa ya habari. Kifungu hiki ndio kitatumika kufanya suala hilo kwa amri ya Waziri. Kifungu hiki pia kinampa Waziri wa Habari mamlaka ya kuelekeza chombo cha habari kutotoa habari Fulani kwa utashi wa Waziri. Ni dhahiri kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa sana wa uhuru wa habari na kuwa kikwazo kikubwa kwa kazi za waandishi. Kwa kutumia kifungu hiki Waziri wa Habari anaweza kuagiza magazeti yote yasiandike habari za IPTL Tegeta Escrow na Waziri atakuwa ndani ya sheria.

Muswada pia unampa Waziri wa Habari mamlaka ya kutoa Masharti ya Kazi za vyombo vya habari ( Terms and Conditions ). Hii inatia nguvu kifungu hicho hapo juu kuhusu maelekezo ya habari za kutolewa na kutotolewa na vyombo vya habari.

Muswada huu umerudisha vifungu vyote kandamizi vilivyopo kwenye sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Kwa mfano kifungu cha 54-56 kinampa Waziri haki ya kutamka kwamba gazeti Fulani au kitabu Fulani kisisambazwe nchini au kuzalishwa nchini. Kwenye masuala mengine Mkurugenzi wa Habari Maelezo na Jeshi la Polisi linaweza kuingia kwa nguvu na kuchukua mitambo inayozalisha magazeti kwa sababu tu gazeti hilo limechapisha habari ambayo kwa maoni ya Serikali ni habari za kichochezi. Muswada umetafsiri uchochezi kuwa ni pamoja na kuandika au kutangaza mambo ambayo yanaweza kutafsiriwa kuwa yanaleta chuki ya wananchi dhidi ya Serikali. Kwa kutumia kifungu hiki, mbunge wa upinzani akihutubia na kuonyesha ufisadi Serikalini, sheria hii inaweza kutumika kufuta vyombo vya habari vilivyoandika au kutangaza habari hiyo.

Kwa ufupi, huu ni muswada mbaya kuliko sheria ya magazeti ya sasa. Huu muswada unairudisha nchi nyuma katika juhudi za kujenga Taifa lenye Haki na wajibu. Ni sheria kandamizi ambazo kama Jaji Francis Nyalali angekuwa hai angeijumuisha katika sheria 40 kandamizi. Serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Taifa lenye giza. Rais Magufuli ameamua kukataa kata kata kuhojiwa na kukosolewa kwa kuhakikisha kuwa anavibana vyombo vya habari nchini. Nilipata kusema huko nyuma kwamba, Serikali ikishamaliza kuvibana vyama vya upinzani itavibana vyombo vya habari. Utabiri ule umetimia kupitia sheria ya huduma za habari inayoelekea kutungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dodoma, 20/10/2016
 http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2016/09/Nape-Nnauye.jpg
Majibu yangu Kwa HOJA za Nape Nnauye kuhusu muswada wa Huduma za habari, 2016

ZITTO KABWE
Ndugu yangu Nape Nnauye amejibu andiko langu nililolitoa Jana kuhusu muswada tajwa. Kama ilivyo ada ya Siasa za kijinga jinga Nape amejibu andiko langu Kwa kunishambulia binafsi na kuweka Hoja zake mbalimbali. Mimi sitamjibu Nape namna yake maana wenye busara wametufunza ' when they go low go high '. Nitajibu Hoja za Nape Na sitamjibu Nape. Hata kwenye andiko langu sikutamka neno Nape Nnauye kwani Siasa zangu sio Siasa za mtu bali za masuala. Sitahangaika Na mtu bali Hoja ili kujenga. 


Hatua ya kwanza ni pale ambapo serikali inapokuwa inatengeneza mswaada husika kabla ya kuupeleka kwenye vikao vya kiserikali kwa hatua za kuupitisha wadau HUSHIRIKISHWA ili kutoa maoni yao. Na kwa mswaada wa Huduma za Vyombo vya Habari ,2016 WADAU wameshirikishwa tena na ushahidi wa maandishi wa ushiriki wao na maoni yao UPO.

Hatua ya pili ya utoaji maoni huwa ni baada ya mswaada kusomwa mara ya KWANZA bungeni, Mswaada husika hukabidhiwa kwa Kamati husika ya Bunge, na ukishakabidhiwa huwa ni waraka huru kwa umma kuusoma na kutoa maoni yao( public document) kwa Kamati ya Bunge. 

Hili pia limefanyika mpaka hatua ya wadau kuitwa na kuja Dodoma ambapo waliomba mbele ya Kamati wapewe muda wakamilishe kazi ya kusoma na kutoa maoni yao. Na Mwenyekiti wa Kamati Ndg. Peter Serukamba(mb) kwa uamuzi wa Kamati ya kudumu ya Bunge wakaamua kuwaongezea muda wadau kwa wiki moja kukamilisha kazi hiyo, shughuli inayoendelea sasa."

Majibu ya Hoja hii

Kanuni za Bunge ( kanuni ya 84 ) zinataka kwamba Muswada ukishasomwa Kwa mara ya kwanza Bunge lifanye MATANGAZO Kwa umma ili kuhakikisha kuwa umma unaelewa maudhui ya muswada na kuwezesha Wananchi kutoa maoni Yao. 

Muswada huu kwanza Bunge halikutoa matangazo yeyote ( Kwa Taarifa tu Ni kwamba Hata Kamati ya Bunge ilishindwa kutoa photocopy nakala za uchambuzi wa muswada kutoka Kwa wanasheria wa Bunge Kwa sababu Bunge halina Fedha. Bunge halina Fedha kutoa photocopy ya nyaraka za Wabunge kufanyia Kazi ). Wadau wote waliokuja mbele ya Kamati ya Bunge walitamka dhahiri kwamba wamepewa Taarifa ya kutokea mbele ya Kamati Siku 2 kabla ya vikao Na hivyo wameomba muda zaidi wa kutoa maoni Yao. Labda Ni kutokana Na uchanga wa shughuli za Bunge, Waziri anajenga Hoja kwamba Ushiriki ulianzia kabla. 

Mtu yeyote anayejua namna Bunge linafanya Kazi atakwambia muswada Ni muswada pale ambapo umechapishwa kwenye gazeti la Serikali Na kusomwa mara ya kwanza Bungeni. Wadau wote waliiambia Kamati kwamba Kwa muswada huu Ndio walikuwa wanashirikishwa Kwa mara ya kwanza pale mbele ya Kamati. Hivyo wadau hawakushirikishwa kwenye muswada huu tangu umesomwa Kwa Mara ya kwanza Bungeni. 

Kama Serikali ina ushahidi wowote ule kwamba kati ya Septemba Na sasa muswada huu umehusisha mdau yeyote waweke wazi uthibitisho huo. Nyaraka zinazoonyeshwa Na Serikali Ni za miaka ya nyuma kabla ya muswada kuwa muswada. Ushirikishaji unaanza rasmi pale muswada upo gazetted Na umesomwa Bungeni. 



#2. Hoja ya kulazimisha vyombo vya Habari nchini kujiunga na TBC:-

"Mosi hakuna kifungu kama hicho katika muswada huu; pili, hakuna dhamira hiyo kwenye muswada huu; na tatu, serikali haina hata wazo hilo."

Majibu ya Hoja 

Itakumbukwa kuwa muswada wa awali ulikuwa Na kifungu hiki Na wadau wakapiga kelele sana kukataa. Ukisoma muswada huu Kwa juu juu utaweza kuona kuwa kifungu hiki hakipo. Mtu mwenye dhamira ovu huficha huficha mambo yake. Kwenye muswada huu mambo mengi yaliyokataliwa Na wadau sasa yamewekwa kiujanja Kwa kuweka Mamlaka hayo Kwa Waziri mwenye dhamana ya Habari. Serikali inaposea hakuna kifungu hicho haisemi kuna kifungu gani. Nitawaeleza kifungu kilichowekwa ambacho ndicho kitatumika na Waziri kufanya haya bila kuhojiwa Na mtu yeyote yule, kupitia kanuni. 

Sehemu ya 7(1)(b)(iv) inatamka wazi kwamba Waziri anaweza kuagiza chombo chochote cha habari cha binafsi kutangaza habari Fulani au masuala Fulani yenye umuhimu kwa Taifa. 
Serikali itatumia kifungu hiki kutekeleza jambo lile lile ambalo wadau walikataa kuwekwa sheria Siku za nyuma. Serikali italiweka Kwa mlango wa nyuma. Mbaya zaidi muswada unatamka wazi kwamba Waziri mwenye dhamana ataweka TERMS and CONDITIONS  Kwa uendeshaji wa ' media houses'. Hivyo Hata wakifuta kifungu Hicho cha 7, bado Waziri kapewa Mamlaka makubwa sana ya kuamua Chombo cha habari kinaendeshwaji. 

Ni dhahiri kwamba Waziri ama anajua haya au kawekewa vifungu ambavyo yeye binafsi hajui tafsiri zake lakini atashangazwa katika utekelezaji wa sheria. Kifungu cha 60(2)(a) ( Minister to make regulations for TERMS and CONDITIONS forOPERATIONS of licensed media house) inampa Mamlaka hayo Waziri kiasi ambacho ataweza kuendesha vyombo vya habari atakavyo yeye. Muswada huu unamfanya Waziri wa Habari kuwa Mhariri Mkuu wa Taifa. 


KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :