Propellerads

Monday, November 14, 2016

mpoma

Afande ahutubia kamati ya bunge kwa sharti la kutoulizwa maswali

Propellerads

Afande ahutubia kamati ya bunge kwa sharti la kutoulizwa maswali



MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la India, Luteni Jenerali Bipin Rawat, amekutana na Kamati ya Bunge ya Ulinzi kwa masharti ya kutoa taarifa bila kuulizwa maswali ya aina yoyote, ikiwamo taarifa husika aliyopaswa kuitoa kwa kamati hiyo.
Kigogo huyo wa jeshi alikutana na kamati hiyo kwa lengo la kutoa taarifa kuhusu operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo wiki mbili zilizopita ndani ya eneo la Pakistani la Kashmir ambalo linakaliwa na jeshi la India kwa madai ya kupambana na makundi ya magaidi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge, Meja Jenerali (mstaafu)  Bhuwan Chandra Khanduri, akizungumzia hali hiyo alisema ni suala la kawaida kwa kuwa taarifa za kina kuhusu masuala ya kijeshi na operesheni zake yanapaswa kuwa siri.
Hata hivyo, Meja Jenerali Khanduri hakueleza ni kwa nini wamemwita afande huyo mbele ya kamati hiyo kutoa taarifa bila kuulizwa maswali ilihali wangeweza tu kutumiwa taarifa hiyo ya maandishi bila uwepo wa kiongozi huyo wa jeshi.  
Meja Jenerali Khanduri alisema ajenda katika ratiba ya kamati yake ilihusu uwasilishwaji wa taarifa fupi tu na kwamba suala la kuwapo kwa maswali na majibu kuhusu taarifa hiyo halikuwezekana kwa kuwa lingeweza kugusa siri za kijeshi.
Hata hivyo, hali haikuwa shwari ndani ya kamati hiyo ya bunge baada ya wabuge kuzuiwa kuuliza maswali. Wabunge wawili ambao ni wajumbe wa kamati hiyo, Ambika Soni na Madhusudhan Mistry pia awali walipinga uamuzi wa jeshi kukataa kufika mbele ya kamati yao kwa ajili ya kutoa taarifa.
Wabunge hao walitoa taarifa yao rasmi ya pamoja kupinga kamati hiyo kukataliwa haki ya kupewa taarifa kwa sababu tu taarifa za kijeshi ni masuala ya siri, wakisema wajumbe wa kamati hiyo wameapa kulinda siri za kamati na masuala mengine nyeti kwa taifa hilo kwa hiyo kuwanyima taarifa kwa madai kuwa taarifa hizo za siri na kwamba zinaweza kuvuja hazina msingi.
Mbunge Madhusudan Mistry alitaka kuuliza maswali lakini juhudi zake hizo zilipuuzwa na Mwenyekiti wa kamati, Meja Jenerali Khanduri.
“Hali ilikuwa tete kiasi cha kurushiana maneno kati ya mbunge huyo na mwenyekiti … lakini hatimaye maswali yalipigwa marufuku,” alisema mbunge mwingine aliyekuwapo kwenye kikao hicho cha kamati.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :