Propellerads

Monday, November 14, 2016

mpoma

Bodi ya Mikopo elimu ya juu nchini yatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu

Propellerads

Bodi ya Mikopo elimu ya juu nchini yatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul - Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wadaiwa sugu wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaadizi wa Ukusanyaji wa Madeni wa Bodi hiyo Dkt. Abdul Mussa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul – Razaq Badru akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wadaiwa sugu wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari, MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaadizi wa Ukusanyaji wa Madeni wa Bodi hiyo Dkt. Abdul Mussa na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.
Dar es Salaam, Tanzania
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa notisi  ya siku thelethini (30) kwa wadaiwa sugu wa mikopo wawe wameanza kulipa madeni yao kabla hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana  na wadai sugu leo Jijini Dar es Salaam.
Badru amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo ya elimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.
Alisema kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walibainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo  kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.
Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimskiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul - Razaq Badru (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia hatua zinazochukuliwa kwa wadaiwa sugu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimskiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Abdul – Razaq Badru (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia hatua zinazochukuliwa kwa wadaiwa sugu leo Jijini Dar es Salaam.
Hatua hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia kuchukua hatua nyingi za ziada.
Hatua hizo ni pamoja na  kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu waziwasilishe, kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.
Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa notisi  ya siku thelethini (30) kwa wadaiwa sugu wa mikopo wawe wameanza kulipa madeni yao kabla hatua zaidi hazijachukuliwa dhidi yao.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)  Abdul – Razaq Badru alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO kuhusiana  na wadai sugu leo Jijini Dar es Salaam.
Badru amesema kuwa notisi hiyo inawalenga wanufaika wa waliokopeshwa na muda wa mataraji ukapita bila wao kuwasilisha taarifa zao na kulipia madaeni ya mikopo ya elimu ya juu waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/95.
Alisema kuwa jumla ya wanufaika 93,500 walibainika na kupelekewa Ankara ya madeni yao ili waweze kulipa hata hivyo  kati yao ni wadaiwa 81,055 ndiyo wanaendelea kulipa madeni yao.
Aidha Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wapo wadaiwa sugu takribani 142,470 wenye mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 239 hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Mussa amesema kuwa urejeshaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 jumla ya shilingi bilioni 25 zimerejeshwa hadi kufikia mwezi Oktoba mwaka huu.
Hatua hii ya kutoa notisi ndani ya siku thelathini inafuatia kutokana na kuvunjwa kwa sheria namba ya 19A (1) cha sheria za Bodi ya Mikopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo pamoja na hatua hiyo Bodi imeazimia kuchukua hatua nyingi za ziada.
Hatua hizo ni pamoja na  kuyatangaza majina ya wadaiwa sugu hadharani ili waajiri, wadhamini wao na wadau wengine wenye taarifa za wasugu waziwasilishe, kuwasilisha majina ya wadaiwa kwenye taasisi zinazotunza taarifa za ukopaji na kukamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.
FacebookTwitterGoogle+WhatsAppPinterestShare
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :