Propellerads

Monday, November 14, 2016

mpoma

Mambo ambayo Trump amewahi kusema juu ya dunia

Propellerads

Mambo ambayo Trump amewahi kusema juu ya dunia


WASHINGTON D.C., MAREKANI
Donald Trump sio mtu wa kukatakata maneno – hata linapokuja suala la kuyazungumzia mataifa mengine.
Baada ya ushindi wake katika uchaguzi mkuu nchini Marekani, Trump sasa ataiwakilisha nchi hiyo katika anga za kimataifa. Lakini ni kwa jinsi gani dunia itampokea? Hapa ni mapitio ya matamshi yake aliyowahi kuyatoa siku za nyuma.
Mexico
Donald Trump ameitaja Mexico mara nyingi katika kampeni zake za kuelekea White House.
Aliyekuwa mgombea wa Republican alitoa matamshi ya kwanza yenye utata, pale alipowaita wahamiaji wa kutoka nchini Mexico “wabakaji” na majambazi. Pia aliahidi “kujenga ukuta mkubwa sana katika mpaka wetu wa kusini. Na nitaifanya Mexico ilipie ukuta huo.”
Mwezi Julai 2015, kupitia ukurasa wake wa Tweeter, aliandika, “Nawapenda watu wa Mexico, lakini Mexico sio rafiki zetu. Wanatuua mpakani na wanatuua kwenye kazi na biashara. PIGANA!”
Trump alikuwa akichanganya matusi na maneno matamu, ikiwemo wakati wa ziara yake ya Mexico kukutana na Rais Enrique Pena Nieto. Lakini inawezekana kukawa na wasiwasi nchini Mexico wakati nchi hiyo inapoamka kwa habari za urais wa Trump.
China
Rais Mteule wa Marekani ameashiria kuwa na msimamo mkali dhidi ya China juu ya masuala ya biashara, kwa kuishutumu nchi hiyo “kuchukua kazi zetu na kuchukua fedha zetu.”
Katika mahojiano mwezi uliopita, Trump alionywa kwamba atakuwa tayari kusitisha mahusiano na China kutokana na jinsi nchi hiyo ya Asia inavyofanya biashara.
“Hawawezi kufanya hilo, kwa sababu kama China ingeweza kufanya hivyo, na kama Marekani ingesitisha uhusiano na China, uchumi wa China utaanguka haraka sana. Namaanisha, China ipo kwa kutegemea fedha kutoka kwa Marekani. Wanashusha thamani ya fedha yao na wanachukua biashara zetu,” alikiambia kituo cha TV cha KSNV.
Wakati Rais Barack Obama alipoitembelea China mwezi Septemba kwa ajili ya mkutano wa G20, Trump alishangazwa na kutokuwepo kwa zulia jekundu kutoka kwenye ndege ya rais wa Marekani ya Air Force One.
“China haijaweka zulia jekundu kutoka kwenye Air Force One na baadae Rais wa Ufilipino anamwita Obama ‘mtoto wa malaya’. Inatisha!
Mara kwa mara amekuwa akiishutumu Beijing kwa kushusha thamani ya fedha yake ili kufanya bidhaa inazosafirisha nje kuwa na bei nzuri zaidi na ametishia kuongeza kodi kwa bidhaa zinazoingia nchini Marekani kutoka China.
Pia amewahi kuishutumu China kwa mashambulizi ya mtandao na kwa kuitumia Korea Kaskazini kwa ugomvi na Marekani.
“China inaidhibiti Korea Kaskazini. Kwa hiyo sasa pamoja na mashambulizi ya mtandaoni, wanaitumia Korea Kaskazini kutusumbua. China ni tishio kubwa,” alisema kwa kupitia mtandao Tweeter mwezi Aprili 2013.

Iran

Trump amekuwa ni mkosoaji mkubwa wa utawala wa Obama juu ya Iran, kwa kusema kuwa mkataba wa kihistoria uliokubaliwa mwaka jana juu ya mpango wa kinyuklia wa Iran “uliipa Iran kiasi cha dola za Kimarekani 150 bilioni na sisi hatukupata chochote – na utakumbukwa kama mkataba mbovu zaidi ambao umewahi kufikiwa.”
“Iran bado inaendelea kuchelewesha makubaliano hayo ya nyuklia wakati ikiendelea kufanya mambo mabaya bila sisi kufahamu. Muda umefika kuachana na mazungumzo nao na kuongeza mara mbili vikwazo dhidi yao. Tuache kuwalipa!” alisema kupitia Tweeter mwaka jana.

Saudi Arabia

Trump hawezi kupata marafiki wengi nchini Saudi Arabia. Alamshambulia Obama kwa kura yake ya veto – ambayo nayo iliondolewa na bunge la seneti – kwa sheria ambayo ingeruhusu familia za waathirika wa mashambulizi ya kigaidi ya 9/11 kuishitaki serikali ya Saudi Arabia, kwa kusema kuwa ilikuwa “aibu na itakumbukwa kama kitu cha aibu kwa urais wake.”
Trump alisema kwamba kama Rais atasaini sheria hiyo. Saudi Arabia iliielezea sheria hiyo kama “inayosikitisha.”
Pia, mwaka 2015, Trump  aliandika kupitia Tweeter kwamba, “Saudi Arabia inapaswa kuilipa Marekani mabilioni mengi ya dola kwa ulinzi tunaowapa. Bila sisi, wasingekuwepo!”
Ujerumani na Ufaransa
Mwezi Januari, Trump aliielezea Ujerumani kama “iliyovurugika” alipokuwa akizungumzia mashambulizi ya kigaidi ya Ujerumani na Ufaransa, na kuyataka mataifa hayo “TUMIA AKILI!”
Katika mahojiano na BBC mwezi Julai, Trump alionyesha kuwa ataweka sheria kali za uhamiaji kwa mataifa hayo mawili, kwa kusema “tuna matatizo nchini Ujerumani na na pia Ufaransa” linapokuja suala la siasa kali za kiislamu. Kinachotakiwa, alisema, ni “kuwafanyia uchunguzi mkali wanaotaka kuja Marekani.”
Uingereza
Mwezi Disemba mwaka jana, Trump aliwakasirisha wengi nchini Uingereza kwa kusema kwamba nchi hiyo ina tatizo kubwa la Waislamu.
Muswada wa umma ulianzishwa baada ya Trump kutaka kupigwa marufuku kwa Waislamu kuingia nchini Marekani na imepata saini za watu wengi – zaidi ya nusu milioni – na kwa kutumia hiyo wabunge nchini Uingereza walifanya majadiliano kuona kama Trump anaweza kuzuiwa kuingia nchini humo kwa kutoa hotuba za chuki. Meya wa London Sadiq Khan, meya wa kwanza wa Kiislamu katika jiji kubwa katika nchi za magharibi, aliiambia CNN kwamba matamshi ya Trumo dhidi ya Uislamu ni ya kipumbavu na kwamba alikuwa akitaka asishinde urais.
Mama yake Trump ni Mskochi na tajiri huyo wa majengo anajulikana kumiliki viwanja kadhaa vya mchezo wa gofu huko Uskochi. Lakini aliwaudhi Waskochi wengi pale alipowapongeza Waingereza baada ya kupiga kura ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Ulaya kwa “kuichukua nchi yao.”

Syria

Trump alisema mwezi machi mwaka huu kwamba Marekani haipaswi kuendelea kuchukua wakimbizi kutoka taifa hilo lenye vita, na kusema kwamba ni tishio kwa “ustaarabu kama ulivyo sasa.”
Miezi minne baadae, aliandika kwenye tweeter “Wakimbizi kutoka Syria wanamiminika kwenye taifa letu. Nani anayefahamu ni akina nani hao – baadhi yao wanaweza kuwa ni ISIS. Rais wetu amechanganyikiwa?”
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :