Propellerads

Wednesday, November 16, 2016

mpoma

MASKINI MTOTO HUYU...........

Propellerads

MASKINI MTOTO HUYU...........

Mtoto huyu anaitwa Hans ni mkazi wa Tabata hapa Dar,siku tatu zilizopita yalikumta makubwa kutoka kwa mama yake wa kambo anaeishinae.Hans alikuja hapa Dar toka mwezi wa tatu akitokea Morogoro kwa mama yake mzazi na kuja hapa Dar kwa baba yake mzazi kwa ajili ya shule na matunzo mengine.Hans kwa sasa ana miaka 9 tu na anasoma shule ya msingi Tabata.

Kama unavyomuona pichani Hans t shirt aliyovaa imetapakaa Damu...
Hans ana mawazo na sura yake haina matumaini ni kama mtu aliyekata tamaa.Wiki iliyopita Hans alitoka shule na shule ilikuwa imefunga akarudi nyumbani na ripoti yake ya mtihani akampa mama yake wa kambo.matokeo yake yalikuwa mazuri maana yupo 10 bora.Baada ya kuingia ndani akabadilisha nguo na akaenda kucheza na watoto wenzie.Baadae mama anamuita na kumfungia chumbani kilichofuata ni kipigo kwa madai kuwa ameiba heha.Hela ambayo Hans hajui ni tsh ngapi inayosemekana kaiba.
Alipigwa mpaka akang'atwa mikononi kama unavyomuona na kifuani,akapigwa mpaka na skuna kichwani na damu zikaanza kumtoka masikioni.Baada ya kupigwa sana majira ya saa moja jioni yule mama akamfukuza nyumbani na Hans akatoka nyumbani pasipokujua hata anakokwenda.
Wakati haya yakitokea baba mzazi hakuwepo,hivyo akaondoka nyumbani hapo kilichotokea majira ya saa nne usiku akaonekana Kipawa akiwa amelala kibarazani kwa mtu aliyetupa habari hii.Ndio kumuuliza kilichotokea na kusimulia yaliyompata mpaka kufika hapo.Ikabidi wamchukue wamlete Tabata ambapo yeye Hans hakuwa
hata akijua ni upande gani wa Tabata alichoshika ni shule anayosoma shule ya msingi Tabata.
Hapo pichani ni alama ya meno kifuani,basi wale walimuokota wakamripoti kwa wajumbe wawili wa eneo la Tabata nao wakamripoti polisi.Kesho yake ikabidi wampeleke shule ili iwe rahisi kuwapata wazazi wake.Kufika shule wakakutana na baba yake mzazi ambae nae alikuwa akimtafuta mwanae.Wajumbe wakamwambia baba inabidi twende polisi tulipotoa ripoti ya kumuokota huyu mtoto...basi walipofika polisi,polisi wakamuweka ndani yule baba wa mtoto wakamwambia mkewe akija pale kituoni ndio watamuachia na kumkamata mke wake kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi vibaya huyo mtoto.
Hapo pichani ni damu zilikuwa zinatoka sikioni na hapo zimeganda.
Hans anasema ni kawaida sana yeye kupigwa na huyo mama wa kambo na mara nyingi humng'ata.
Kichwani ni majeraha yaliyotokana na kupigwa na skuna....duuh yaani huyu mama sijui alikuwa kamdhamiria nini mwana wa mwenzie???!!!

Hans alipatiwa matibabu,mpaka sasa sijui kinaendelea nini tutafatilia halafu tutakwambia nini kilijiri baada ya hapo.

Asante Gea kwa picha na pia wiki hii utaisikia habari hii katika hekaheka za leo ndani ya leo tena.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :