Rais Dkt.Magufuli Awasili Mkoani Singida Pia Anatarajia Kushiriki Katika Ibada ua Krismas Siku ya Kesho Tarehe 25/12/2016 Mkoani Humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili mkoani humo. Pia Rais Dkt. Magufuli anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Krismasi mkoani humo hapo Kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida. (Picha na Ikulu)