Propellerads

Saturday, October 29, 2016

mpoma

30 wapoteza maisha

Propellerads

Watu 30 wapoteza maisha na wengine 94 wamejuruhiwa baada ya kutokea mlipuko wakiwa katika harusi

Licha ya juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na serikali ya Syria na mataifa mengine ili kuhakikisha serikali ya nchi hiyo inakibidhibiti kikundi cha ISIS na sehemu kuwa salama kwa raia wake, hali bado ni tete.
Mashambulio ya kigaidi yanayo endelea nchini Uturuki na Syria kumekua na mfululizo wa milipuko ya mabomu ya kujitoa muhanga na matukio ya kigaidi katika mji wa Gaziantep, ulioko pembezoni mwa mipaka ya Syria.
Jana usiku wakati wa harusi moja mjini humo, kulisikika milipuko ya amabomu katika maeneo ya katikati ya mji wa Gaziantep na kusababisha vifo vya watu 30 na kujeruhi wengine 94.
Serikali ya uturuki imelitambua tukio hilo kama shambulio la kigaidi na kusema kwamba lilikua limefanywa na watu wa kujitoa muhanga.
Serikali ya nchi hiyo imesema kwamba bado haija julikana nani ni muhisika katika tukio hilo, lakini ina hatihati kua shirika la kiislam (IS) ambao ndio wana makazi katika mipaka ya Gaziantep na Syria.
Uturuki imekua ikikumbwa na mfululizo wa mashambulizi ya mabomu kutoka kwa vikundi vya kiislam na majeshi ya Kurdish kwa kipindi cha mwaka ulio pita, bila kusahau tukio la mwisho mwezi wa tano katika uwanja wa ndege wa instanbul na kuua watu 40.
Kikundi cha Jihadist hivi karibuni wamepoteza makazi kwa kushambuliwa na wanajeshi wa Syria kaskazini mwa Syria ikiwemo kiongozi wao Manbij, huku majeshi ya Syria yakiendelea kuongeza nguvu katika kupambana na vikundi vya kiislam vya Jarablus. Kama mlipuko huu ni wa kikundi cha kiislamu, basi ni dhairi kwamba ni shambulio la kulipiza kisasi.
Mwandishi wa BBC kutokea Gazientep alisema kwamba “shambulio limejotokeza katika mji ambao umekua kutokana na yanayo endelea katika mipaka” lakini limekua la kushangaza zaid kwani mpka harusi ilikua imelengwa.
“Harusi nchini uturuki zina chukuliwa kama kitu cha muhimu na cha furaha sana, lakini kuibadilisha kua siku ya hudhuni inatengeneza hofu kubwa sana kwao” alisema mwandishi huyo.
KUPATA KAZI POPOTE NCHINI BONYEZA 'HAPA' CHINI. Propellerads

mpoma

About mpoma

Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.

Subscribe to this Blog via Email :