Mtoto wa Miaka minne Auawa, Atupwa Kisimani
Mtoto wa kike, Rahila Salim Ali (4) amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umening’inizwa kisimani na vidole vya mikono vikiwa vimekatwa na mashavu kuchubuliwa. Tukio hilo limetokea jana asubuhi, katika eneo Njiapanda, Mbagala, Temeke baada ya mtoto huyo kutoweka nyumbani siku nne zilizopita. Akizungumzia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo, Raziah Ramadhani alisema binti yake alitoweka...