ANGALIA PICHA AJALI YA COSTA- WATU ZAIDI YA 25 WAJERUHIWA HUKO MBEYA,DEREVA ANUSA KIPIGO CHA ABIRIA
Watu zaidi ya 25 wajeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jana baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Costa kutoka Mbozi kuelekea Mbeya kupinduka katika eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya.
Kwa mujibu wa baadhi ya majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo walisema chanzo ni dereva kushindwa kulimudu gari la abiria baada ya kulikwepa gari dogo kutokana na kuwa na mwendokasi pamoja na mvua kubwa iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Baadhi ya majeruhi wakitoka ndani ya basi hilo |
Baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospitali teule ya Ifisi na wengine wakipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya matibabu zaidi.
Baadhi ya abilia wakitaka kumpiga Dereva wagari ya aina ya Suzuki kuwa yeye ndio alisababisha ajali hiyo kwa kuyumbayumba kwake barabarani |
Moja ya wasamaria wema akiwazuia abiria wenye hasira kali kutaka kumpiga mzee huyo Mwenye Suzuki ambae alijulikana kwa jina moja tu mzee Mtawa |