WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA SPAIN NCHINI.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo leo Septemba 30,2016 wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwa Waziri Jijini Dar es Salaam kukabidhi moja ya mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanywa na serikali ya Spain katika Bonde la Ufa la Olduvai Gorge Mkoani Manyara.
Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kuhusu kuendeleza mradi wa kujenga Shule ya Mpira wa Miguu Kigamboni kama ilivyokuwa katika mkakati wa awali alipofika Ofisini kwa waziri Jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016 kumkaribisha kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Utamaduni yaliyoandaliwa na nchi ya Spain yatakayofanyika Makumbusho ya Taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akisoma mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanyika Olduvai Goerge mkoani Manyara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) walipokuwa wakifanya mazungumzo Ofisini Jijini Dar es Salaam kuhusu kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo Septemba 30, 2016