TAARIFA ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE OFISI YA MBUNGE JIMBO LA MIKUMI
Mkulima mmoja aitwaye OMARY SULULU mapema Leo tar 1 January 2017 ameshambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa na panga kichwani na mfugaji kwenye kijiji cha MAMOYO kata Ya MABWEREBWERE Jimbo La Mikumi. Tukio hilo limetokea baada ya Ndugu OMARY SULULU alivyokuwa akijaribu kufukuza mifugo hiyo kwenye mashamba ya Migomba, nyanya na Mahindi, Kwa sasa Ndugu OMARY SULULU anaendelea na Matibabu katika Hospitali Ya Wilaya Ya Kilosa.
Juhudi zilizokwishafanywa na Mhe Mbunge ameweza kuwasiliana na Mkuu wa Wilaya Ya Kilosa kwa hatua zaidi
Lakini pia Mbunge wa jimbo La Mikumi Mhe JOSEPH LEONARD HAULE anaendelea kutoa wito na kuiomba sana serikali itusaidie kutatua migogoro hii isiyokwisha ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA...